Shirika la Anga la Etihad (EAG) limetangaza uteuzi wa Gavin Halliday kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hala Group ikiwa ni sehemu ya kuboresha utendaji wake na kuimarisha huduma zake ulimwenguni.

Halliday ataliongoza shirika hilo katika kuendana na huduma bora ulimwenguni ikiwa ni pamoja na kuwasogeza karibu wateja na kuendelea kufurahia huduma bora zinazotolewa na shirika hili pamoja na washirika wake wa ndege. Pia, atawajibika kuwa karibu na wabia wa EAG pamoja na kushiriki vikao vya utawala ambavyo ni ndiyo nguzo muhimu kwa mipango na maendeleo ukuaji wa biashara ya usafirishaji Abu Dhab na Nchi za Falme za Kiarabu.

Halliday anaungana na Shirika la Anga la Etihad baada ya kufanya kazi na kuwa na uzoefu mkubwa akifanya kazi kwa miaka 30 katika Shirika la Ndege la Etihad na kwenye Shirika la IAG. Kwa miaka mitatu ya hivi karibuni amekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Avios, ambayo ni programu maarufu ulimwenguni. Pia amewahi kuwa katika nafasi ya juu akihusika na masuala ya biashara kwenye Shirika la IAG, Iberia, British Midland na British Airways.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Anga la Etihad, H.E Mohomed Mubarak Fadhel Al Mazrouei alisema, “Hala ni nembo muhimu kwa Etihad ambayo imekuwa ikihakikisha inawaunganisha wabia wetu kwenye biashara ya usafiri wa anga. Pia ni idara muhimu ambayo imekuwa kiungo muhimu kwa wasafiri wa Abu Dhab na Nchi za Famlme za Kiarabu kwenye biashara na usafirishaji wa uhakika. Gavinni ni miongoni mwa watu muhimu kwenye sekta hii ya usafiri wa anga, hivyo tunafurahia kujiunga na timu ya uongozi wa EAG.

“Tumefurahishwa na uzoefu wa Gavin na tunaamini ataendeleza programu za masoko ulimwenguni jambo ambalo ndiyo mpango wetu mkubwa.”
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hala Group Gavin Halliday .

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...