BENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 10 kwa timu ya Singida United kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakayoendelea kuanzia mwezi Agosti mwaka huu.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali, Richard Makungwa alisema msaada huo umelenga kusaidia timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa kwa ligi hiyo.

"Tumetoa msaada huu kwa timu ya Singida United kwa kwa ajili ya maandalizi ya ligi hiyo na hii ni kawaida yetu kusaidia timu mbalimbali pale tunapopata nafasi" alisema Makungwa.

Makungwa alisema licha ya benki hiyo kufanya shughuli za kibenki pia imejikita kuinua michezo nchini kwa kutoa msaada wa vifaa vya michezo.

Alitaja vifaa walivyotoa msaada kwa timu hiyo ni viatu vya mpira wa miguu, jezi na mipira vyote vikiwa na thamani ya sh.milioni 10.

Katibu wa timu hiyo Abdurahman Sima alisema vifaa hivyo walivyopata vitatumika kwa lengo lililokusudiwa na si vinginevyo."Tunaishukuru benki ya NMB kwa msaada huu tunaomba wadau wengine kuiga mfano wa benki hii " alisema Sima.
Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Richard Makungwa (kulia), akimkabidhi Katibu wa Timu ya Singida United, Abdurahman Sima,  mipira na vifaa vingine vya michezo vyenye thamani ya sh,milioni 10 Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakayoanza Agosti mwaka huu.
Katibu wa Timu ya Singida United, Abdurahman Sima (kushoto), akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupokea vifaa hivyo.
Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Richard Makungwa (katikati), akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo. Kulia ni Mwenyekiti wa timu hiyo, Yusuph Mwandani.
Vifaa vilivyokabidhiwa vikioneshwa kwa wanahabari. imeandikwa Na Dotto Mwaibale.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...