THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

STAR TIMES YAINGIA UBIA NA TPB KUUZA LUNINGA ZA KIDIJITALI KWA MKOPO

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Kampuni ya startimes imeingia ubia na benki ya TPB kwa lengo la kuwakopesha wateja televisheni za kidigitali kwa awamu kupitia mkopo ambao utamwezesha mteja kulipa mpaka miezi kumi na miwili kutoka benki ya TPB.

akizungumza na Waandishi wa habari jijini dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa mpnago huo Makamu wa Rais wa Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal, amesema kuwa ubia huo unamwezesha mteja wa startimes kulipia kwa njia rahisi zaidi televisheni ya kidigitali sio tu kwa mara moja bali kwa awamu kupitia Benki ya TPB.

"wateja wataweza kuipata huduma hii katika mikoa mitano ambayo ni Dar es salaam, Dodoma, Mwanza Arusha na Mbeya ambapo kuna matawi ya Benki hiyo" amesema Zuhra.

Akiongea katika uzinduzi, Meneja Mahusiano wa StarTimes, Antony Katunzi amesema ushirikiano huu unaashiria wazi mapinduzi ambayo Benki na Kampuni ya Televisheni zinaweza kuleta, kwa kurahisisha ulipiaji kwa wateja wao na jamii kwa ujumla ili kuwezesha kila familia kumiliki luninga ya kidigitali ya StarTimes.

Naye Amos Kasanga, Meneja Masoko wa Benki ya TPB amesema benki hiyo imekubaliana na StarTimes kutoa mikopo hiyo midogo kwenye mikoa mitano ambapo huduma hiyo itapatikana. Njia hii ni rahisi zaidi kwa wateja kutumia.

“Najisikia furaha kubwa leo tunapozindua njia nyingine ambayo inazileta pamoja kampuni hizi kubwa mbili Tanzania, na hii itatoa fursa kwa wateja na kila familia ya kitanzania kumiliki luninga ya kidigitali na kufurahia maisha ya kidigitali kwa kupata vipindi mbali mbali kutoka kila kona ya dunia”

Kwa hatua hii, wateja na wasio wateja wa StarTimes, wote wanaweza kulipia luninga za kidigitali za StarTimes kwa awamu kupitia matawi ya Benki ya TPB. 

Watanzania waishio mijini na vijijini sasa wataweza kumiliki luninga za kidigitali kwa urahisi, kulingana na mahitaji na uwezo wao kifedha.

Tunayo matoleo mbalimbali ya luninga za kidigitali kwa ajili ya wateja wetu kulingana na mahitaji na uwezo wao. Tuna luninga ya inchi 24 kwa Tsh. 45,000/=,kwa kila mwezi kwa miezi kumi na miwili (12),inchi 32 Tsh 64,000/= na inchi 40 kwa Tsh. 99,000/= .
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal akikata utepe kwa pamoja na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya Mikopo ya Luninga za kisasa kwa kushirikiana na Star Times.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal wakifungua kitambaa kwa pamoja na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya kuashiria uzinduzi wa huduma za mikopo ya Luninga za Star Times Kupitia benki ya Posta.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya wakionyesha moja ya Luninga zitakazokuwa zinakopeshwa kupitia benki ya Posta.
Baadhi ya watumishi wa kampuni ya StarTimes Tanzania ambao wamehudhuria sherehe hiyo.