Taasisi na Asasi Zisizokuwa
za Kiserikali za Tanzania (NGOs) taasisi za serikali zinazoshughulikia
uwajibikaji na wadau wengine kadhaa walikutana hivi leo ili kufanya tathmini ya hatua zilizopigwa na
mafunzo yaliyopatikana wakati wa uhai wa mradi wa Pamoja Twajenga unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia
Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID). Toka mwaka 2013,
watendaji wa mradi wa Pamoja Twajenga wamekuwa
wakifanya kazi bega kwa bega na asasi za kiraia na taasisi za serikali ya
Tanzania zinazoshughulikia masuala ya uwajibikaji ili kuimarisha mahusiano kati
ya asasi za kiraia na serikali. Mradi huu ulitoa mafunzo na msaada kwa jumla ya
asasi zisizo za Kiserikali 16 na taasisi tatu za serikali zinazojihusisha na
uwajibikaji katika mikoa ya Mtwara, Iringa, Dodoma, Morogoro na Zanzibar kwa lengo la kukuza uwazi na
uwajibikaji wa serikali kwa raia wa Tanzania.
Kutokana
na msaada huu, hivi sasa asasi za kiraia na taasisi za uwajibikaji
zilizoshiriki zina uwezo zaidi wa kushiriki katika mijadala kuhusu masuala
mahsusi yanayozigusa jamii (issue-based dialogue). Raia katika mikoa lengwa ya mradi – ikiwa ni ni pamoja na vijana, wanawake na makundi mengine ya watu wanaowekwa pembezoni wana uwezo zaidi wa kujadiliana na serikali zao kuhusu kero zao, jambo ambalo limeongeza uwajibikaji na uwazi katika usimamizi wa rasilimali za umma na katika ufanyaji maamuzi. Asasi za kiraia zilizosaidiwa na mradi wa Pamoja Twajenga zinafanya kazi katika masuala yanayohusiana moja kwa moja na mahitaji ya msingi ya raia ikiwa ni pamoja na huduma za afya, elimu, usalama wa chakula na usimamizi wa rasilimali. |
Majadiliano ya jumuiya katika kata ya Mpapula mkoani Mtwara, mwanajamii akielezea uzoefu wao kuhusu vitendo vya ukatili vinavyofanywa dhidi ya wanawake na watoto. Majadiliano hayo yaliandaliwa na asasi ya kiraia ya Wanasheria Wanawake Katika Maendeleo Afrika (Women in Law and Development in Africa - WiLDAF), mojawapo kati ya asasi za kiraia zilizopokea msaada kutoka mradi wa Pamoja Twajenga uliokuwa ukifadhiliwa na USAID. (Picha kwa hisani ya: Rhoda Nashon/WiLDAF) Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA |
Home
Unlabelled
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...