Mshauri wa Taasisi ya Mama’s & Papa’s For Community
Reform Rehabilitation Center (MPFCR) Balozi Patrick Chokala akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu utoaji wa TUZO kwa baadhi ya watu wenyemkachango
katika jamii leo Jijini Dar es Salaam. Tuzo hizo zitatolewa tarehe 12 mwezi
huu. Watakaopewa tuzo hizo ni Dkt. Reginald Mengi, Mchungaji Dkt. Getrude
Rwakatale, Mhe. Agustino Lyatonga Mrema, Mustafa Sabodo, na Mohamed Gulam
Dewji. Kulia ni Mjumbe wa Taasisi hiyo Omary Kombe.
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva ambaye pia ni
Balozi wa Taasisi ya Mama’s & Papa’s For Community Reform Rehabilitation
Center (MPFCR), Nurdin Bilal maarufu kama Shetta (baba Kaira) akielezea jambo
mbele ya waandishi wa habari kuhusu yeye kuwa Balozi wa Taasisi hiyo kwa lengo
la kuunga mkono jitihada za kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya leo Jijini
Dar es Salaam.Taasisi hiyo pia imetoa Tuzo za heshima kwa baadhi ya watu wenye
mchango katika jamii. Kutoka kulia ni Mshauri wa Taasisi hiyo Balozi Patrick
Chokala na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bibi. Emmi Ally Ghahae.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia
mkutano wao na wawakilishi wa Taasisi ya Mama’s & Papa’s For Community
Reform Rehabilitation Center (MPFCR) leo jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo
inatarajia kutoa Tuzo za heshima kwa baadhi ya wadau wanajali na kuthamini
jamii.Watakaopewa tuzo hizo ni Dkt. Reginald Mengi, Mchungaji Dkt. Getrude
Rwakatale, Mhe. Agustino Lyatonga Mrema, Mustafa Sabodo, na Mohamed Gulam
Dewji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...