Na Pascal Mayalla 
 Taasisi ya TradeMark East Africa inazijengea uwezo bidhaa za Tanzania ili  kuziingiza kwenye masoko ya kimataifa, kwa kuziwezesha kukidhi viwango vya ubora wa kimataifa.
Kwa hatua hiyo bidhaa hizo zitakuwa na uwezo wa kuhimili ushindani wa kimataifa na kuingia kwenye masoko ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bara la Afrika na masoko ya kimataifa yakiwemo masoko ya Ulaya na Marekani, amesema Mkurugenzi wa TradeMark Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga kwenye kongamano ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es salaam Jumamosi.
Bw. Ulanga amesema zoezi la kuhakikisha bidhaa za Tanzania zinafikia viwango vya ubora wa kimataifa, linafanywa kwa kupitia mafunzo ya viwango vya ubora kwa kuzitumia taasisi za TBC, TFDA na GS 1 kwa ajili ya barcode kwa bidhaa za Tanzania, hivyo bidhaa hizo kuweza kuhimili ushindani katika masoko ya kimataifa kwa kukidhi viwango vya ubora wa kimataifa. 
 Bw. Ulanga amesema mafunzo hayo yanaendeshwa kwa awamu mbalimbali, ni sehemu ya utakelezaji wa mradi mkubwa wa Taasisi ya Trademark East Africa ujulikanao kama “Women in Trade” unaolenga kuwajengea uwezo wafanyabiashara wanawake wa Tanzania, kuhimili ushindani wa kibiashara na kukabiliana na vikwazo vya kibiashara kwa wafanyabiasha wanawake Tanzania kuwawezesha kufanya biashara ya kimataifa ikiwemo kuwezesha bidhaa zao kuyafikia masoko ya nchi za Afrika Mashariki na masoko ya kimataifa ambapo Taasisi ya TradeMark imetenga Dola za Marekani zaidi ya Milioni 5,300,000 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 12 za Kitanzania kugharimia mpango huo.
Mwenyekiti wa TWCC, Mama Jaquline Maleko akizungumza.
Mkurugenzi wa TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, John Ulanga akizungumza kwenye hafla fupi  ya kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukidhi viwango vya kimataifa vya ubora wa bidhaa, kwa Wafanyabiashara wanawake  wa Tanzania yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) ili kuwezesha bidhaa za Tanzania, kuyafikia masoko ya Afrika Mashariki nay a kimataifa. Mafunzo hayo, yameendeshwa na SIDO kwa kushirikiana na taasisi za TBS, TFDA na GS 1 na kufadhiliwa na TradeMark East Africa. Kushoto ni Mwenyekiti wa TWCC, Mama Jaquline Maleko 
 Washirika wa mafunzo hayo,

 Washirika wa mafunzo hayo,
Washirika wa mafunzo hayo, 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...