THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TADB, TAHA WAPANGA KUSAIDIA SEKTA YA MALI MBICHI NA MATUNDA (HORTICULTURE)


Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) na Asasi Kilele ya wakulima wa Malimbichi na Matunda Tanzania (TAHA) zinajipanga kusaidia sekta Malimbichi na Matunda (horticulture) ili kuongeza tija kwa kilimo hicho.

Watendaji wakuu wa taasisi hizo wamesema kuwa kuna haja ya makusudi ya uwekezaji mkubwa katika sekta ya Malimbichi na Matunda (horticulture) ili kuchagiza na kusaidia mapinduzi katika sekta hiyo na kilimo kwa ujumla nchini.

“Tunajipanga kuchochea ukuaji wa sekta hii ili kuwakwamua wakulima wa malimbichi kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini,” anasema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa ushirikiano kati ya TADB na TAHA kwa kuwa taasisi zote ni za Kilele (apex institutions) zenye kulenga katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kutoka kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha kibiashara na uzalishaji wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
 
Timu ya Maandalizi ya Makubaliano ya ushirikiano katika kuisaidia sekta ya malimbichi na matunda nchini wakiwa katika majadiliano.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Francis Assenga (kulia) akimuelezea Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi (hayupo pichani) nafasi ya TADB katika kuleta mapinduzi ya kilimo nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara, Augustino Chacha. 
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Francis Assenga (kushoto) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi (kulia) nafasi ya TADB katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAHA, Jijini Arusha. 
Timu ya Maandalizi ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya TADB na TAHA katika kuisaidia sekta ya malimbichi na matunda nchini wakiwa katika majadiliano wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano wao. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAHA, Jijini Arusha.