Wito umetolewa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuchangamkia fursa za uwekezaji katika serkta ya kilimo na mifugo kwa kuwapatia mikopo wakulima wanaojishughulisha katika sekta hizo.

Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega wakati akizungumza na ugeni kutoka TADB walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha.

Bw. Kwitega amesema kuwa mkoa wa Arusha una fursa nyingi za uwekezaji hasa katika maeneo ya kilimo na ufugaji.

Akizungumza wakati wa mazungumzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga alisema uanzishwaji wa TADB unatokana na Serikali kutambua umuhimu wa uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya Kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo.

Bw. Assenga mkoa wa Arusha utaingizwa rasmi katika mpango wa biashara wa Benki na ametoa wito kwa wakulima na wafugaji wa mkoa wa Arusha kuchangamkia fursa zinazotolewa na TADB.
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (kushoto) akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kulia) wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha.
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (katikati) akizungumza na ugeni kutoka TADB wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha. Ugeni uliongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...