NA ALLY DAUD-WAMJW.

TANZANIA bado haijafikiwa na ugonjwa wa ebola kama inavyodaiwa na baadhi ya watu kutokana na utafiti uliofanyika na wataalamu wa afya hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya  Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu tishio la uwepo wa ugonjwa huo katika nchi za jirani .

“Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu bali wachukue tahadhari zaa kujikinga na ugonjwa huu kwani mpaka sasa hakuna mtu aliyethibitishwa kuugua ugonjwa huu hapa nchini” alisema Dkt. Ulisubisya.

Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa watanzania  hususani wanaoishi mikoa ya karibu na nchi yaa Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo ikiwemo Mwanza,Kagera,Kigoma,Rukwa, Katavi na Songwe wanatkiwa kuwa makini kwani ugonjwa wa ebola  upo nchini humo.

Dkt. Ulisubisya amesema kuwa ugonjwa wa ebola unasababishwa na kugusa majimaji yanayotoka kwa mgonjwa mwenye ebola na mizoga  na dalili za ugonjwa huo  zinatokea`baada siku mbili pindi mgonjwa anapopata maambukizi y ugonjwa huu zikiwemo kutokwa na damu sehemu za puani,masikioni na homa kali.

Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa  Wizara imechukua hatua za kutoa mafunzo mbalimbali kwa watoa huduma za afya ,kuandaa  kituo cha kuhifadhi  wagonjwa na`kutibu ugonjwa wa ebola kilichopo wilaya ya temeke kwa wagonjwa wanaotokea mkoa wa  Dar es salaam na kutoa vipimo vya joto la mwili kwa wasafiri ili kutambua ugonjwa huo.

Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya amesema kuwa Wizara itashirikiana na sekta mbalimbali za afya ili kupata mbinu za kudhibiti ugonjwa huo na Wananchi wanashauriwa kutoa taarifa na kupata elimu kuhusu ugonjwa wa Ebola kupitia namba 117 bilaa y malipo kwa mitaandao yote.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza na waandishi wa habari  (hawapo pichani) juu ya Wananchi kutokuwa na hofu bali wachukue tahadhari za kujikinga na ugonjwa wa ebola kwani mpaka sasa hakuna mtu aliyethibitishwa kuugua ugonjwa huu hapa nchin leo jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wa Afya,waandi wa habari  wakimsikiluliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Mpoki Ulisubisya leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel  Massaka, Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...