Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde inaeleza kuwa Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo wa Jimbo la Moshi Mjini na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Kilimanjaro, Mzee Philemone Ndesamburo amefariki Dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya KCMC, Mkoani humo. 

Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amethibitisha muda huu juu ya kifo hicho na kwamba bado haijafahamika chanzo cha kifo chake.

Kwa sasa mwili wa marehmu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti hospitali ya rufaa ya KCMC .

Ndugu wakiwemo watoto wa marehemu wamefika Hospitalini hapo na kuomba mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi kutokana na kifo kuwa ni cha ghafla.

Lema alisema, Mzee Ndesamburo alifika ofisini kwake majira ya asubuhi na alionekana mwenye afya njema, ilipofika majira ya saa nne hali ilibadilika na kushindwa kuendelea na majukumu yake.

Ndipo walipomkimbiza KCMC kwa ajili ya matibabu na alifariki dunia akiwa kitengo cha emergency, Taarifa zaidi tutajulishana kadri zitakapokuwa zikitufikia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...