THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TFF YAVITAHADHALISHA VYOMBO VYA HABARI KUACHA KAMPENI CHAFU


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limevionya Vyombo vya Habari ambavyo vinaripoti habari zenye lengo za kuichafua shirikisho hilo na viongozi wake .

Hayo yamesemwa na Afisa habari wa TFF Alfredy Lucas alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,  juu ya tuhuma zilizotolewa na moja ya gazeti la kila siku.

“Navitaka baadhi ya vyombo vya habari nchini kuacha mara moja kampeni za upotoshaji zenye lengo la kuwachafua viongozi wa juu wa shirikisho la soka hapa nchini.Amesema Alfred Lucas.

Amesema TFF imeshtushwa na taarifa inayoendelea kutolewa kwenye gazeti moja la kila siku ikidai kuwa kuna ufisadi ndani ya shirikisho wakati madai hayo ni ya uongo na yenye lengo la kujenga mtazamo hasi dhidi ya shirikisho na viongozi wake.

Ametaja kuwa Gazeti hilo la kila siku limetumia taarifa ya ukaguzi wa fedha iliyofanywa na wakaguzi kutoka TAC kujenga picha kuwa ni ushahidi tosha wa kuwepo kwa ufisadi ndani ya shirikisho.

Ameweka wazi kuwa taarifa ya ukaguzi wa fedha ya TAC haikuwahi kuituhumu TFF kwa ufisadi. Taarifa ilibaini maeneo ya kiuhasibu ambayo yalihitaji maelezo ya ziada ya namna baadhi ya malipo yalivyofanyika (audit queries), na ufafanuzi ulitolewa kwa ufasaha na watendaji wa shirikisho na kupelekwa mbele ya Mkutano Mkuu wa Shirikisho.

Amesema hata hivyo gazeti hilo ambalo limeonekana kuweka kando kabisa misingi ya uandishi wa habari, limechapisha taarifa bila hata kutoa nafasi kwa wanaotuhumiwa kujibu na kutoa ufafanuzi stahiki.

“Rais na katibu mkuu wa shirikisho wanahudhuria mikutano ya CAF nje ya nchi wakati gazeti hilo likiendelea kuporomosha mlolongo wa tuhuma bila kutoa haki ya kusikilizwa kwa wanaoandikwa vibaya, TFF inaliangalia suala hili kama kampeni chafu inayofanywa ili kushawishi matokeo ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Agasti mwaka huu.” Amesema Alfredy Lucas.

Pia taarifa hii potofu inalenga kulihamisha taifa kutoka kwenye masuala ya msingi kama kuiunga mkono Serengeti Boys kwenye mashindano ya Afrika na kuanza kujadili masuala yanayohusiana na siasa za uchaguzi wa TFF.

TFF kwa sasa inatafakari hatua za kisheria za kuchukua dhidi ya vyombo vya habari husika na inachukua nafasi hii kuvisihi vyombo vya habari kuacha mara moja kujihusisha na kampeni ya kuchafuana ambayo ni kinyume na misingi ya maadili ya uandishi wa habari.

Afisa habari wa TFF Alfredy Lucas
Waandishi wakifatili akatika mkutano huo