Benki ya TIB Corporate imeingia ubia na TRA kwa kuunganisha mifumo yao ya malipo ili kuwezesha kulipa kodi kwa urahisi.
TAXBANK Ni mfumo wa kisasa wa ukusanyaji wa kodi ambao umerahisisha ulipaji  wa kodi kwa wateja wetu. Kwa kupitia utaratibu huu Bank imeunganisha mfumo wake wa malipo moja kwa moja na mfumo wa TRA, hivyo mlipa kodi akilipia katika tawi lolote la bank, taarifa zake zinaonekana mara moja katika mtandao wa TRA hivyo kumuwezesha mlipa kodi kuendelea na taratibu zingine kwa haraka na  kiurahisi zaidi. 
TIB Corporate Bank Ltd (TIB CBL) ni benki ya  biashara inayomilikiwa na Serikali kwa 100%. Benki inatoa huduma zote za kibenki za kibishara kwa  mashirika na taasisi za aina mbalimbali za serikali na  binafsi , pia benki inatoa huduma kwa watu binafsi.
Benki ina matawi  6 kwa sasa,  Dar es salaam (3), Mwanza , Arusha na Mbeya. 
Benki inatoa huduma mbalimbali  kutokana na mahitaji ya mteja. Baadhi ya  huduma hizo ni pamoja na; akaunti za aina mbalimbali kwa makampuni na watu binafsi, mikopo ya aina mbali mbali ya muda mfupi na wa kati, Dhamana za Kibenki(Guarantees),Uuzaji na ununuaji wa fedha za kigeni, ushauri wa uwezekaji katika hati fungani,ukusanyaji wa fedha na kuwezesha malipo ya jumla kwa makampuni pamoja na ulipaji wa mishahara kwa njia rahisi na ya haraka
Huduma zote hizi hutolewa kwa umahiri na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha mteja anafurahia mahusiano yake na benki. 
Benki imejiunga na mfumo  huu wa ulipaji kodi, ili kusaidia kufanikisha malengo ya serikali katika kuongeza ufanisi katika kukusanya kodi. Kwa kupitia mfumo huu mlipa kodi anapata huduma bora zaidi pamoja na faida zifuatazo:
·         - Kumrahisishia mlipa kodi  kufanya muamala wa kulipa kodi kwa haraka na ufanisi.
·         - Kupunguza uwezano wa makosa katika ulipaji wa kodi
·         - Kupunguza ghrama za uendeshaji na miamala.
TIB Corporate ndio yenye dhamana ya kusimamia sehemu kubwa ya  akaunti za mamlaka ya Bandari-TPA. Tayari tunalo tawi dogo ndani ya bandari ili kuhakikisha kuwa tunawezesha ulipaji wa kodi zote na tozo za bandari kwa ukaribu. Kutoa huduma za kibenki kwa masaa 24 sambamba na agizo la raisi wetu Mhe. John Pombe Magufuli kuzitaka taasisi husika katika bandari kutoa huduma kwa masaa 24.
 Mkurugenzi Mkuu wa  TIB Corporate Bank Bw. Frank Nyabundege akizungumza jinsi bank ilivyojipanga kutoa huduma hiyo
Kamishna Jenerali  wa TRA Bw.Charles Kichere akikabidhiana mkataba na mkurugenzi mkuu wa TIB Corporate Bank Bw. Frank Nyabundege. Wakishuhudiwa na mkurugenzi wa huduma na elimu kwa wateja wa TRA Bw. Richard Kayombo na Mkuu wa Kitengo na Masoko na mahusiano ya Kampuni wa TIB Corporate Bi. Theresia Soka
 Wafanyakazi wa TIB Corporate wakifurahia baada ya kusaini mkataba Frank Nyabundege- Mkurugenzi mkuu,  Bi.Theresia Soka – Mkuu wa masoko na mahusiano ya Kampuni, Bi. Bahati Minja- Mkurugenzi wa matawi na huduma kwa wateja, Bw. Mwallu Mwachang’a –Mkurugenzi wa biashara
 Kamishna Jenerali wa TRA Bw. General Charles Kichere akizungumza juu ya mpango huo
Mkurugenzi Mkuu wa  TIB Corporate Bank Bw. Frank Nyabundege akizungumza jinsi bank ilivyojipanga kutoa huduma hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...