Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Mfuko wa Sekta Binafsi Nchini (TPSF) umesema kuwa katika kujenga mazingira ya biashara kunahitaji kuwepo kwa sekta ya umma pamoja na sekta binafsi katika kuandaa maeneo tengefu ya biashara.

Hayo ameyasema leo Makamu Mwenyekiti wa TPSF, Salum Shamte kwa niaba ya Mwenyekiti wa TPSF wakati akifungua mkutano wa 17 wa mwaka wa Mfuko wa Sekta ya Binafsi (TPSF) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Shamte amesema kuwa katika kuendana na mipango ya kufikia uchumi wa kati sekta binafsi na sekta ya umma zinatakiwa kushirikiana katika kuangalia mazingira ya kufanya uwekezaji wa viwanda. 

Amesema katika maagizo ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa wakuu wa mikoa , kutenga maeneo ya viwanda ambapo kuna uwezekano huo upo lakini changamoto ni miundombinu ya maeneo hayo.

Aidha ameiomba serikali kuanizisha Benki ya kuendeleza viwanda ili sekta hiyo iweze kukua na kufikia uchumi wa kati kwa kuajili watanzania wengi.
Shamte ameimba serikali kuongeza bajeti kwa mamlaka ya EPZA ili kuweza kutenga maeneo tengefu ya viwanda.

Hata hivyo amesema kuwa sekta binafsi ndio inaajiri kwa sehemu kubwa kuliko sekta ya umma, kutokana na takwimu zinaonesha kwa mwaka vijana wanahitimu 800,000 kwa sekta ya umma inaajiri vijana 40,000. 

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye amesema mkutano 17 kwa majadiliano yatayofanyika yataongeza uhai wa TPSF .Amesema ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi unazidi kuimarika hivyo kunaleta tija juu mahusiano.
Makamu Mwenyekiti wa TPSF, Salum Shamte akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa 17 wa Mfuko wa Sekta Binafsi nchini uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akikaribisha wajumbe wa mkutano mkuu wa mfuko huo leo katika uliofanyika katika ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa EPZA ,Joseph Simbakalia akiwasilisha mada katika mkutano mkuu wa 17 wa TSPF, uliofanyika katika ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.
Sehemu wajumbe wa Mkutano 17 wa TPSF uliofanyika katika ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...