SHIRIKA la Trust Care Tanzania Foundation kwa
kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wameandaa semina ya kuwajengea
uwezo wa kifikra wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam
ikiwa na lengo la kuwabadili wanafunzi kwa ujumla kuwa na mawazo chanya
yatakayowawezesha kutumia fursa anuai zinazowazunguka katika jamii mara baada
ya masomo yao.
Akizungumzia semina hiyo inayotarajiwa kufanyika Jumamosi ya
tarehe 20/05/2017 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam
(DUCE) kuanzia majira ya saa tatu asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care
Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu alisema semina hiyo ni maalum kwa wanafunzi
waliopo vyuoni kwa ajili ya kuwajengea uwezo.
Alizitaja mada ambazo wanafunzi
wanatarajia kufundishwa ni pamoja na Umuhimu wa Kujiamini na Kujijengea Uwezo,
Uwezo wa Uthubutu, Vipaji na Jinsi ya Kuviendeleza, Maadili na Nidhamu katika
Kazi na Ubunifu katika Kufikia Malengo. “Semina inawaandaa vijana waliopo na
ambao wanatarajia kumaliza elimu yao ya juu hivi karibuni kupata elimu na ujuzi
utakaowasaidia wakiwa shule na baada ya kumaliza masomo yao ili waweze kwenda
sambamba na mahitaji ya ulimwengu wa sasa…” alisema Bw. Mbwafu.Akifafanua zaidi Mkurugenzi, Zambert Mbwafu, alivitaja vyuo
vitakavyoshiriki katika semina hiyo; ni pamoja IFM, CBE, DIT, DUCE, TIA, UDSM,
MUHAS, CHUO CHA DIPLOMASIA, KIU, CHUO CHA USTAWI WA JAMII NA CHUO KIKUU CHA
TUMAINI.
Mkurugenzi
wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Injinia Enocent Msasi
akizungumza katika mkutano na wanahabari leo kuzungumzia semina ya wanavyuo
inayotarajia kufanyika Jumamosi ya tarehe 20/05/2017 katika ukumbi wa Chuo
Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE) kuanzia majira ya saa tatu asubuhi.
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert
Mbwafu na Ofisa Masoko wa Kampuni ya TTCL, Lulu Kamalamo (kulia) wakiwa katika
mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania
Foundation, Zambert Mbwafu akizungumza katika mkutano na wanahabari leo
kuzungumzia semina ya wanafunzi wa vyuo vikuu inayotarajia kufanyika Jumamosi
ya tarehe 20/05/2017 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam
(DUCE) kuanzia majira ya saa tatu asubuhi. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara wa
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Injinia Enocent Msasi akiwa katika mkutano huo
Mkurugenzi wa Elimu na Utafiti wa
Trust Care Tanzania Foundation, Fadhila Nyoni akifafanua jambo juu ya semina ya
wanafunzi wa vyuo vikuu katika mkutano na wanahabari leo. Kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu akifuatilia mazungumzo
hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...