Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
UCHAGUZI wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu (TAFCA) Mkoa wa Kinondoni uliokuwa ufanyike Mei 7 mwaka huu jijini Dar es Salaam sasa umesogezwa mbele hadi Juni 4.
Uamuzi wa kusogeza mbele uchaguzi huo umetokana na mwitikio mdogo wa uchukuaji fomu kwa wagombea. Muda wa uchukuaji fomu sasa umeongezwa hadi Mei 7 mwaka huu.
Fomu kwa ajili ya wagombea zinatolewa kwenye ofisi za Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni (KIFA) kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni.
Ada ya fomu kwa wagombea wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TAFCA ni sh. 50,000 wakati Mhazini, Mhazini Msaidizi na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni sh. 30,000.
Ajenda ya uchaguzi itatanguliwa na Mkutano Mkuu wa Kawaida ambao mbali ya taarifa ya utendaji, Kamati ya Utendaji inayomaliza muda wake pia itawasilisha ripoti ya mapato na matumizi.
Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA Kinondoni inaongozwa na Mwenyekiti wa zamani wa TAFCA, Ramadhan Mambosasa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...