Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya nchini inamshikilia mmiliki wa kampuni ya Techno Net Scientific kwa kuingiza kemikali bashirifu nchini zenye ujazo wa lita 6494 kwa kukiuka sheria na taratibu.
 Imeelezwa kuwa, mmiliki huyo amekiuka sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya namba 5 ya 2015 na ile usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani, sheria ambayo inasimamiwa na Mkemia mkuu wa Serikali.
Kamishna Mkuu wa mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na dawa za kulevya Rogers Sianga amesema kuwa, Kukamatwa kwa mmiliki wa kampuni hiyo, yenye makazi yake eneo la mwenge kunatokana na taarifa walizopata kutoka kwa raia wema mwezi uliopita waliowataarifu kuwa kampuni hiyo inaagiza kemikali bashirifu, ambazo ni hatari kwa matumizi na zisiporatibiwa zinaweza kutumika vibaya na kuleta madhara.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo, baada ya ziara fupi ya kutembelea maghala mawili ya kampuni  hiyo yanayotumika kuhifhadhia kemikali hizo, Sianga amesema, uchunguzi wao umeonyesha kuwa, kampuni hiyo inaagiza kemikali bila kibali.

“Tulichogundua ni kwamba kampuni hii ya Tecno Net Scientific yenye makazi yake eneo la mwenge, imeagiza kemikali nyingi ambazo ni bashirifu, kemikali bashirifu ni kemikali muhimu kwa utengenezaji wa kawaida wa dawa za binadamu lakini pia zikichepushwa  zikiwa diverted zinaweza kutengeneza dawa za kulevya za Heroine, Cocaine na nyinginezo ambazo huzalisha kemikali taka zenye sumu ambazo zinaweza kuhatarisha afya za watu na kuchafua mazingira.
  Kamishna Mkuu wa mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na dawa za kulevya Rogers Sianga, akizungumza na Waandishi wa habari juu ya athari za Dawa hizo ambazo zilikamatwa katika moja ya Maghala huko Mwenge 
Kamishna Msaidizi wa  Mamlaka ya Kupambana na Dawa Bertha Mamuya akitoa ufafanuzi  juu ya  kemikali bashirifu zinavyoweza kuchepushwa kwa matumizi mengine
Kamishna Msaidizi wa  Mamlaka ya Kupambana na Dawa Bertha Mamuya akionesha baadhi ya Maghala kwa ndani sehemu ya ghala ya kuhifadhi Dawa.
Kamishna Msaidizi wa  Mamlaka ya Kupambana na Dawa Bertha Mamuya akionesha ghala la pili la kuhifadhi Dawa ambapo wamebaini kuwapo kwa dawa zilizomaliza muda wake.
Sehemu ya  nje ya jengo la kampuni ya  Tecno Net Scientific  ambalo lilitumika katika kutengenezea na kuhifadhi madawa hayo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...