THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

ULEGA AWATEMBELEA WANANCHI WA TAMBANI WALIOKOSA MAWASILIANO BAINA YA KIJIJI NA KIJIJI

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amewatembelea wananchi wa Kijiji Tambani ambao hawana mawasiliano ya kuvuka kwenda kutokana na daraja kuchukuliwa na maji.

Akizungumza na wananchi cha Tambani, Ulega amesema kuwa mvua hizo zimeleta athari hivyo unahitajika ufumbuzi wa haraka.

Amesema usafiri wa mitumbwi si salama katika kutoa huduma ya usafiri kwa wananchi wa kijiji cha tambani na maeneo mengine. Kutokana na wananchi hao kukosa mawasiliano Mbunge huyo ametoa sh.milioni moja pamoja na mifuko ya saruji 100 ili kuweza kutengeneza daraja hilo.

Wananchi wa kijiji hicho kwa kila kaya wamekubalina kutoa sh.10,000 ambazo zitafanya kazi katika ujenzi wa daraja hilo pamoja na nguvu zao zitatumika. Diwani wa Tambani, Ally Mtamilwa amsema kuwa ujio wa Mbunge wa jimbo la Mkuranga ameeta matumaini kwa wananchi na kuahidi nae kutoa mifuko 20 ya saruji.
Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa katika kivuko ambacho si salama kuelekea upande wa pili alipotembelea kijiji cha tambani ambao wamekosa mawasiliano leo.

Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akikabidhi msaada wa sh.milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa daraja lilichukuwa na maji katika kijiji cha Tambani.
Wananchi wakisubiri kivuko ambacho si salama na kuwagharimu kulipa sh.500 kwa kila safari wanayoifanya kwenda katika vijiji vingine kupata mahitaji .(picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii )
Diwani wa Tambani , Ally Mtamilwa akizungumza na wananchi wake wakati wa ziara ya mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega.
Wananchi wa wa kijiji cha Tambani ambao wamekosa mawasiliano kutokana na daraja kuchukuliwa na maji,wakimsikiliza Mbunge wao Mh. Abdallah Ulega aliekwenda kuwatembelea na kujionea hali halisi na leo.