THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Upelelezi kesi ya Masogange wakamilika

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Baada ya mahakama kutoa  hati ya kukamatwa Video  Queen Agnes Gerald maarufu kama Masogange (28) kwa kushindwa kutoka mahakamani mara kadhaa, hatimae leo  amejisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mapema mwezi uliopita, mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilitoa amri ya kukamatwa kwa mshtakiwa Masogange kwa kushindwa kuhudhuria mahakamani mara mbili katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili.

Hatua hiyo ya kutaka kukamatwa kwa Masogange  ilikuja baada ya upande wa mashitaka katika shauri lililopita, kuomba mahakama hiyo kutoa hati ya kumkamata kutokana na mshitakiwa huyo pamoja na wadhamini wake kutofika mahakamani, licha ya kupewa onyo.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri alikubali maombi hayo na kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa ambaye ni Masogange.

Hata hivyo, Masogange amefika mahakamani hapo leo mapema na alipoulizwa na Hakimu Mashauri sababu za kumfanya yeye kutofika mahakamani, amedai kuwa alifika lakini alichelewa.

Wakilli wa serikali Shadrack  Kimaro, ameieleza mahakama kuwa upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na ameiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali(PH).

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 13 mwaka huu kwa ajili ya PH.
Awali ilidaiwa kuwa,

Masogange anakabiliwa na tuhuma za kutumia dawa za kulevya aina ya heroin diacety na Oxazepam.

Awali ilidaiwa kuwa, kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, maeneo yasiyofahamika jijini Dar es Salaam,  Masogange alitumia dawa za kulevya aina ya heroin (diacety/morpline) kinyume na sheria.
Aidha anadaiwa, kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam