Na Lorietha Laurence-WHUSM.

Dhana ya kuwekeza katika sekta ya michezo kwa vijana wadogo wa shule za Sekondari imekua ikileta manufaa makubwa kwa Taifa katika kuzalisha wachezaji mahiri ambao wamekua wakipeperusha bendera ya Tanzania ndani na nje ya chini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe alipokua akifungua michezo ya COPA UMISSETA ambayo inashirikisha shule za Sekondari za Serikali na Binafsi leo katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

“Nimefurahishwa na juhudi zinazofanywa na Kampuni ya CocaCola katika kuhakikisha tunaimarisha sekta ya michezo kwa vijana wadogo wa sekondari kwani kwa kufanya hivyo tunaibua vipaji na kuviendeleza kwa  kupata  wanamichezo mahiri wa baadaye” amesema Waziri Mwakyembe.

Aidha aliongeza kuwa Serikali itahakikisha kuwa inawekeza katika michezo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa kuwa michezo ni ajira inayowapatia vijana riziki pamoja na kuchangia katika uchumi wa nchi.

Vilevile aliwataka walimu kufuata ratiba za vipindi vya michezo kwa kuhamasisha michezo mashuleni ikiwemo kuwapatia wanafunzi nafasi ya kujifunza na sio kuvitumia vipindi hivyo kwa shughuli nyingine.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akiimba wimbo wa Taifa wakati wa kufungua mashindano ya COPA UMISSETA uliofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yussuph Singo na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya CocaCola Eric Ongara na anayefuatia ni Rais wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) Bw.Vitalus Shija.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akiongea na wanafunzi wa shule za Sekondari za Jijini Dar es Salaam wakati wa kufungua kwa mashindano ya COPA UMISSETA katika uwanja wa mpira wa Taifa.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia) akisalimiana na washiriki wa michezo ya COPA UMISSETA inayoshirikisha shule za Sekondari za Serikali na Binafsi iliyofunguliwa leo Jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...