Wajasiriamali wa Kilimanjaro Vicoba Network (KIVINET) wamepata elimu ya ujasiriamali baada ya kupata mafunzo yaliyoandaliwa na FINCA Microfinance Bank mjini Moshi mwishoni mwa wiki.

“Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha wajasiriamali wa KIVINET kuwa na uelewa wa kutosha wa kukuza miradi na mitaji yao hivyo kushiriki kikamilifu katika kukuza uchumi”, alisema Mkurugenzi wa biashara wa FINCA Microfinance Bank Bw. Gershom Mpangala.

KIVINET inajumuisha zaidi ya wanachama 10,000 kutoka vikundi mbalimbali mjini Moshi ambavyo vimesaidia kuwawezesha kushiriki katika fursa za kiuchumi na kuwawezesha kuboresha biashara zao na kuinua kiwango cha maisha yao. “Mafunzo haya yametuwezesha kubadilishana mawazo na kupeana uzoefu. Naamini sasa watafanya biashara zao mafanikio zaidi”, alisema Mpangala.

Katika mafunzo hayo, maofisa wa Finca waliweza kutoa ufafanuzi wa huduma ambazo wanaweza kupata na masuala ya kutilia manani katika kukuza biashara zao. “Tumejaribu kuwaonyesha mikopo yetu ya elimu ambayo imeandaliwa maalum kwa ajili ya kumsaidia mjasiriamali na namna ya kuepuka kuvuranga mtaji wake pale ambapo anatakiwa alipe karo ya mtoto wake,’ alisema Mpangala.

Naye Meneja wa Benki ya FINCA Mkoani Kilimanjaro Sebastiani Timothy amesema wao wanahusika na utoaji wa elimu ya ujasiriamali pamoja na mikopo yenye riba nafuu kwa wajasiriamali wadogowadogo na wale wa kati lengo likiwa ni kuhakikisha wanaweza kujikwamua kiuchumi. Vikundi vya Vicoba kwa hapa Moshi tunawahudumia sana kwa sababu mbali na kuwapa mikopo yenye riba nafuu lakini pia tunatoa elimu jinsi ya kutunza fedha na pia jinsi ya kufanya biashara kwa mafanikio, aliongeza Timothy.

Kwa upande wake, Matia Mathiasi Mwingira ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Kilimanjaro Vicoba Network (Vicoba) amesema ni vigumu kwa wafanyabiashara kufanikiwa bila kupata mikopo yenye riba nafuu hivyo ni vyema taasisi za kifedha zikatoa mikopo yenye riba nafuu ili wajasiriamali waweze kumudu na kuboresha maisha yao. ‘Nawapongeza sana Benki ya Finca kwani licha ya kusikia kilio chetu sisi Vicoba na kuamua kutupatia mikopo nafuu lakini pia wanatupa mafunzo bure ya jinsi ya kutumia vyema mikopo yetu, alisema Mwingira.

Mwingira pia ametoa wito kwa akinamama ambao hawapo kwenye vikundi vidogo vidogo yaani VICOBA kujiunga ili wapate fursa za mikopo ikiwepo mikopo kwa ajili ya ada za shule.

Wanachama wa Kilimanjaro VICOBA Network (KIVINET) wakiwa kwenye mafunzo ya jinsi ya kutumia mikopo wanayopata kutoka FINCA Microfinance Bank. Mafunzo hayo yaliandaliwa na benki hiyo na kufanyika mjini Moshi mwishoni mwa wiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...