Baada ya kukaa kimya kwa miezi kibao bila kuachia wimbo, Hussein Machozi ameachia
wimbo mpya uitwao, Nipe Sikuachi. Wimbo huo umetayarishwa na mshindi wa tuzo ya
mtayarishaji bora wa Bongo Flava katika miaka tofauti, Man Walter kupitia studio zake
za Combination Sound.
“Combination yangu ya mimi na Man Walter, sidhani kama kuna kitu cha mchezo hapo,”
anasema Machozi kuhusiana na wimbo huo.
“Man Walter ni mshkaji kitambo, tumekutana tukakubaliana kufanya kazi na tukaona
kabisa kwamba sisi tukifanya kazi wawili itakuwa kazi na ndicho kilichofanyika,”
ameongeza.
Anaeleza, “Video pia imefanyika Italy, Gressoney Italy. Kuna mabadiliko makubwa
ukiangalia location ambazo tumezizoea, ukiangalia video ambazo kila siku tunaziona
Tanzania za magari na majumba.”
Machozi ambaye anafahamika kwa vibao vingi vilivyowahi kufanya vizuri kwenye vituo
vya redio na runinga ndani na nje ya Tanzania vikiwemo ‘Utaipenda’, ‘Kwaajili Yako’,
‘Addicted’ na zingine, amedai kuwa ukimya wake ulitokana na majukumu mengine ya
kimaisha.
“Kama unavyojua, hakuna mtu anapenda kuwa kimya, na ukifuatilia vizuri kuna kazi
kadhaa nilishawahi kuziachia lakini hazikufika nilikotarajia nadhani kwasababu ya
ukosefu wa management.
Kwa sasa Hussein anaishi nchini Italia baada ya kuwa ameenda kusoma, lakini hiyo
haimaanishi kuwa ameupa kisogo muziki, kitu anachoamini alizaliwa kukifanya.
“Kinachokuja kuonekana sasa hivi, hakijawahi kuonekana katika macho ya watu na
nimejaribu kufanya hivyo kwasababu mimi mwenyewe nahitaji mabadiliko, nifanye kitu
ambacho ni kipya zaidi hata kwenye macho yangu mimi, kwahiyo nimekikubali kwamba
ni kipya, video ni mpya, audio ni mpya kabisa.”
Video ya wimbo huo ipo Youtube tayari na audio itapatikana mtandaoni
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...