Wadhamini wa kuu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC inatarajia kutoa zawadi kwa washindi wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa 2016/2017 siku ya Jumatano.

Pamoja na kutoa zawadi mbali mbali kwa timu washiriki, kampuni hiyo ambayo ni mdhamini mkuu wa ligi, imezipongeza timu zote zilizoshiriki msimu huu wa ligi na itatoa zawadi kwa timu ambazo zimefanikiwa kushika nafasi ya kwanza hadi ya tatu.

Meneja uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, kampuni ya Vodacom inafurahi kuona msimu wa ligi ukimalizika kwa mafanikio makubwa huku timu ya Yanga ikiweza kuibuka mshindi kwa miaka miwili mfululizo.


“Tunaipongeza timu ya Yanga pamoja na mshindi wa pili na wa tatu,Ligi ilikuwa na msisimko pamoja na ushindani mkubwa,” alisema

Nkurlu aliongeza, “waswahili husema chanda chema huvishwa pete, tunapenda kuwatangazia wadau wa soka na timu zilizoshiriki ligi kuu kuwa tarehe 24 siku ya Jumatano tutakuwa na sherehe kubwa itakayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city ya kukabidhi zawadi yao mabingwa. Pamoja na mabingwa, timu nyingine zilizoshiriki zitaweza kuzawadiwa zawadi mbali mbali kwa kuwa zawadi zao zipo tayari pia kamati Maalum iliyoundwa kusimamia tuzo hizi imefanya mabadiliko kiasi kwa kuongeza baadhi ya tuzo ambazo hazikuwepo msimu uliopita lengo ikiwa ni kuboresha tuzo hizi.

Tuzo zilizoongezwa ni: Tuzo ya Heshima (ambayo itatolewa kwa mwanasoka nguli wa zamani mwenye historia nzuri kwa soka la Tanzania).”
Alisema Vodacom Tanzania mwaka huu imetoa zawadi mapema kwa kuwa ni utaratibu wa kawaida kwa kampuni hiyo kukabidhi zawadi mara tu baada ya msimu wa ligi kwisha.

“Uchelewaji wa kutoa zawadi hutokana na sababu mbali mbali ambazo zinakuwaga nje ya uwezo wao ikiwamo baadhi ya timu kuwa zinashiriki mashindano mengine kama Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Sababu nyingine ni pamoja na mfungo wa mwezi mtuku wa Ramadhani,” alieleza Meneja Uhusiano huyo.

Nkurlu alisema utoaji wa zawadi mapema pia utazisaidia timu kuwa na muda wa kutosha kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujoa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...