THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Wachimbaji madini wadogo wawili wapoteza maisha mgodini Iringa

  Na MatukiodaimaBlog 
WACHIMBAJI wawili  wadogo wa madini ya dhahabu katika kijiji cha Masuluti kata ya Magulilwa tarafa ya Mlowa wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamefariki dunia baada ya kukosa hewa wakiwa kazini ndani ya mgodi.
Afisa mtendaji wa kijiji cha Masuluti Venjaslaus Kiunosile amesema kuwa tukio hilo  limetokea leo Majira ya saa  5 asubuhi, na kwamba taarifa ya tukio hilo alipewa na mchimbaji mwenzao aliyewatembelea marehemu hao kwa ajili ya kuwasalimia. 
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Julius Mjengi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa miili ya marehemu hao imetolewa katika mgodi huo. Aliwataja waliofariki dunia kwa kukosa hewa kuwa ni Haus Kaijage (32) mkazi wa Bukoba na James Mlawa(22) mkazi wa Magulilwa.
Alisema chanzo cha watu hao kupoteza maisha ni kukosa hewa baada ya kuingiza jenereta la kuvuta maji mgodini kwa lengo la kuvuta maji, na baada ya kuliwasha walikosa hewa.
Alisema alisema wachimbaji hao walichukua mashine hiyo na kuiingiza ndani na mgodi baada ya awali kuharibika na kuwa jeshi la polisi linamshikilia kwa mahojiano mmiliki wa mgodi huo Samweli Msigwa.
Kamanda Mjengi alitoa wito kwa wachimbaji wadogo katika mkoa wa Iringa kuzingatia usalama katika uchimbaji wa madini.
Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mgama Dkt Baraka Mwifune alisema uchunguzi alioufanya unaonyesha  watu hao walipoteza maisha kwa kukosa hewa.
Mmiliki wa mgodi huo Samweli Msigwa alisema kuwa akiwa njiani kuelekea eneo la mgodi kwa ajili ya kusaidia kutengeneza mashine ya kuingiza hewa katika mgodi huo ndipo alipopata taarifa ya wachimbaji hao wawili kati ya Sita kupoteza maisha kwa kukosa hewa. 
Alisema mgodi huo ulikuwa na wachimbaji sita kabla ya wanne kwenda mgodi mpya wa Ismani na hivyo walibaki hao wawili na kuwa anamiliki mgodi huo kihalali na ana kibali kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.
 Kamanda  wa  polisi  mkoa  wa Iringa  Julius Mjengi kushoto akitazama shimo la mgodi  katika  kijiji  cha Msuluti  kata ya Magulilwa wilaya ya Iringa ambalo wachimbaji  wawili  wadogo wawili  walipoteza maisha kwa  kukosa  hewa wakati  wakichimba madini jana asubuhi
 Mmiliki wa mgodi huo Samweli Msigwa (kulia) akihojiwa na polisi. Katikati ni kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julius Mjengi 
 Kamanda  wa  polisi  mkoa  wa Iringa  Julius Mjengi kushoto akikagua mazingira wa  mgodi huo  katika  kijiji  cha Msuluti  kata ya Magulilwa wilaya ya Iringa ambalo wachimbaji  wawili  wadogo wawili  walipoteza maisha kwa  kukosa  hewa wakati  wakichimba madini jana asubuhi
Wananchi wa Msuluti kata ya Magulilwa   wilaya ya  Iringa  wakiwa wamebeba mmoja kati ya  miili ya  wachimbaji  wadogo  wawili  waliokufa mgodini kwa  kukosa hewa  leo.