THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Wachimbaji wadogo waiomba Serikali kutoa elimu ya uchimbaji bora

Mchimbaji mdogo wa Madini ya Almas ambaye pia ni Mshauri Mwelekezi wa SANA Gems Gregory Kibusi, akiangalia ubora wa Madini ya Alams.

Na Asteria Muhozya, Arusha

Wachimbaji wadogo wa Madini walioshiriki Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito, Arusha wameiomba Serikali kuendelea kutoa elimu ya uchimbaji bora na uhifadhi wa mazingira kwa wachimbaji nchini.

Ombi hilo lilitolewa na Mshauri Mwelekezi wa Kampuni ya SANA Gems, ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa madini ya Almas, Gregory Kibusi. Kampuni ya SANA Gems inayofanya shughuli zake za uchimbaji mkoani Shinyanga ndiyo kampuni pekee ya wachimbaji wadogo iliyokuwa ikionesha madini ya Almas katika Maonesho hayo.

Kibusi aliongeza kuwa, ushiriki wa wachimbaji katika maonesho hayo ni fursa kwao ya kukutana na wanunuzi na kujenga mtandao wa kibiashara hivyo kuiomba serikali kuendelea kuwahamisha wachimbaji wadogo nchini kushiriki katika maonesho hayo kwa kuwa, yanawezesha uhakika wa masoko ya madini yao.

"Nikiwa pia kama Katibu Mkuu wa wachimbaji wadogo Shinyanga, natoa wito kwa wachimbaji nchini kutumia vyama vyao washiriki maonesho haya ya Arusha kwa kuleta madini yao. Soko la uhakika lipo," alisema Kibusi. Aidha, Kibusi alitumia fursa hiyo kuwataka wachimbaji nchini kuachana na matumizi ya zebaki na kuwataka kutumia njia bora zinazoelekezwa na Serikali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ravi Hasmukh, alisema kuwa, kampuni hiyo imeshiriki Maonesho hayo ili kuweza kujenga mtandao wa kibiashara ikiwemo pia kutoa fursa kwa Watanzania kujifunza namna Madini ya Almas yanavyochimbwa na mahali yanapopatikana. Aidha, ameitaka Serikali ifikishe umeme katika eneo hilo na maeneo mengine mbapo shughuli za uchimbaji mdogo zipofanyika ili kuwezesha kuharakisha maendeleo ikiwemo kuwezesha shughuli za kiuchumi na kupanua wigo wa ajira.

Akizungumzia namna kampuni hiyo inavyosaidia eneo linalozunguka mgodi wake alisema kuwa, kampuni hiyo imetengeneza kisima cha maji kwa ajili ya kijiji cha Hukiro pamoja na kuboresha baadhi ya miundombinu katika zahanati iliyo jirani na mgodi wa kampuni hiyo Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Vito Arusha yalifunguliwa rasmi tarehe 3 Mei na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel Bendera na kufungwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Mshauri Mwelekezi wa SANA Gems Gregory Kibusi, (kulia), akionesha madini ya Almas . Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ravi Hasmukh. Kulia ni Mkurugenzi Mwenza Kishan Bhatti.
Madini ya Almas ambayo bado hayajasanifiwa.