THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Wafanyakazi NMB kuchangia upasuaji wa watoto wenye mdomo Sungura

Baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha Corporate Support cha NMB wakipiga picha na mmoja wa wanufaika wa wanufaika wa upasuaji wa mdomo Sungura uliotolewa na wafanyakazi wa kitengo cha Corporate Support cha Benki ya NMB.

 WAFANYAKAZI wa Benki ya NMB katika kitengo cha Corporate Support wamedhamini upasuaji wa watoto wanne wenye midomo Sungura waliokuwa wamelezwa katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam. Akizungumzia udhamini huo, Meneja Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Majengo NMB, Elizabeth Lukaza alisema ufadhili huo ni sehemu ya utaratibu ambao wamejiwekea wao kama wafanyakazi wa kitengo cha Corporate Support kusaidia jamii kwa sehemu yenye uhitaji.

Alisema ufadhili huo ulikuwa wa Dola 1,200 (Tsh. 2.6 milioni) na hiyo siyo mara ya kwanza wao kutoa ufadhili kwa kuchangia huduma mbalimbali za kijamii kwani kila mwaka hufanya hivyo angalau mara tatu. 

“Kila mwaka tunatoa msaada kwa jamii, kwa mwaka huu tumekuja CCBRT tumesaidia watoto wanne ambao walikuwa wanatakiwa kufanyiwa upasuaji wa mdomo Sungura, upasuaji wa kila mtoto tumetao Dolla 300," “Pesa hizi tumejichangisha katika kitengo na ofisi imetuchangia sehemu ya fedha ili kufanikisha lengo letu, tumekuwa tukifanya mambo mbalimbali, tumewahi hata kutoa damu kwenye kituo chao kilichopo Mwananyamala,” alisema Elizabeth. Mmoja wa wanufaika wa ufadhili wa wafanyakazi wa kitengo cha Corporate Support cha NMB, Emmanuel Isdor (mtoto), akiwa amebebwa na mama na mamae, Maines Ephrahim.[/caption] Pia alizungumzia mipango ya kitengo chao kwa siku zijazo, “Kuna vitu vingi vya kufanya, kama kitengo chetu tumemua kuunga mkono juhudi za benki kupitia kitengo cha masuala ya uwajikikaji kwa jamii (CSR). 

Pia tutaendelea kufuatilia maendeleo ya afya za watoto hawa kupitia wazazi wao,” Naye mmoja wa wazazi ambao mtoto wake amefanyiwa upasuaji wa mdomo Sungura kwa ufadhili wa NMB kupitia kitengo cha Corporate Support, Maines Ephrahim alionyesha Furaha na kuwashukuru NMB kwa ufadhili huo na kueleza kuwa kabla ya upasuaji huo hali ya mtoto ilikuwa tofauti na ilivyo sasa. 

“Nawashukuru NMB kwa msaada ambao wamempatia mtoto wangu (Emmanuel Isdor), amefanyiwa upasuaji vizuri…kabla ya upasuaji mtoto alikuwa analialia, lakini sasa hali ni nzuri nimefurahi,” alisema Maines. Kwa upande wa nesi aliyewahudumia katika wodi ya watoto wenye mdomo sungura na walemavu, Joyce Cosmas alisema, “Nawashukuru NMB kwa msaada waliotoa, kwa sisi kama manesi tuliwapokea vizuri na kuwapa huduma zote ambazo walikuwa walistahili kuzipata.”