Mdahalo wa televisheni wa baada ya duru ya kwanza na kabla ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa ulifanyika Jumatano, Mei 3, mjini Paris. Wagombea urais wawili Emmanuel Macron na Marine Le Pen ndio walishiriki mdahalo huo.

Wagombea hao, kila mmoja alitoa sera zake kwa kuwashawishi wale ambao bado hawajaonyesha msimamo wao wa kupiga kura. Emmanuel Macron na Marine Le Pen walishambliana kwa maneno makali.

Wagombea katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa walikabiliana vikali katika mdahalo wa televisheni uliofanyika Jumatano Mei 3. Emmanuel Macron na Le Pen walipambana kwa muda wa zaidi ya saa 2 na dakika 30 katika mdahalo wa baada ya duru ya kwanza na kabla ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais. Marine Le Pen mgombea kwa tiketi ya chama cha FN, ambaye alichukua nafasi ya pili baada ya kushindwa na Emmanuel Macron alionekana kumshambulia mpinzani wake kuanzia mwanzo wa mdahalo huo.

Bi Le Pen alisema Emmanuel Macron ni "mgombea wa utandawazi wa kikatili, wa ukatili wa kijamii, wa vita vya wote dhidi ya wote". "Mkakati wako ni kusema tu uongo, lakini haupendekezi chochote," alijibu Emmanuel Macron, akijitetea.

Mdahalo huo uligeuka na kuchuku sura nyingine ambapo wagombea hao wawili walijibizana vikali, kila mmoja akimshambulia mwenginei. Bii Le Pen alimstumu mpinzani wake kuhusu masuala makubwa ya viwanda kama sera ya kiuchumi na kijamii. "Wewe unatii mahitaji ya Umoja wa Ulaya, ushindani usio wa haki za kimataifa (...) huna ujasiri wa kitaifa, haufikirii maslahi ya taifa," Marine Le pen amesema.

Ziara ya kiwanda cha Whirlpool katika mji wa Amiens tarehe 26 Aprili ilirejelewa katika mdahalo huo na kuzua mvutano mkubwa. Emmanuel Macron amemtuhumu mpinzani wake kuwa "alichukulia maisha ya dhiki yanayo wakabili wafanyakazi wa kiwanda hicho kwa kutetea maslahi yake." "Mimi sijajificha" katika mkutano na shirikisho la wafanyakazi, alijibu Bi Le Pen. "

Katika mdahalo huo wagombea waligusia maswala ya usalama na ugaidi. bi Le pen amesema " inabidi kurejesha mipaka yetu, kufukuza wageni kukwama katika nchi yetu, kuwanyima wageni uraia" alisema Marine Le Pen, kabla kumshutumu Emmanuel Macron kuwa anarahisisha ugaidi wa Kiislamu ".

Emmanuel Macon alijitetea kwa kuhakikisha kuwa tishio la kigaidi ni "kipaumbele" kwake. "Kama amiri jeshi mkuu, kama mkuu wa usalama, nitafanya mapambano kwa pande zote dhidi ya ugaidi wa Kiislamu, " amesema Bw Macron.chanzo RFI 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...