Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa miradi yote yenye thamani isiyozidi bilioni 10 wapewe Wakandarasi wa ndani hasa kwa miradi inayotekelezwa kwa fedha za ndani kwani wakandarasi hao watasaidia kuongeza ajira kwa vijana wa Kitanzania na kuongeza uwekezaji ndani ya nchi.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mjini DODOMA wakati anafungua mkutano wa siku Mbili wa mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi mwa mwaka 2017.

Makamu wa Rais amesisitiza wakandarasi hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili na sheria pamoja na kumaliza kazi wanazopewa ndani ya muda uliopangwa kwa kuzingatia ubora wa kazi na gharama zilizokubalika kwenye mikataba na sio vinginenevyo.

Makamu wa Rais amewataka wakandarasi kote nchini kuacha mara moja tabia ya kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wanayopewa.
Amesema kuwa Serikali itaendelea kuwapa kipaumbele wakandarasi wazawa ili wathubuti kujitosa na kumudu zabuni za ujenzi kwani kwa kufanya hivyo kutaleta faida mbalimbali ikiwemo fedha watakazopata watawekeza ndani ya nchi na kutoa ajira za kutosha kwa vijana wa Kitanzania.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
 Wajumbe  wa Mkutano wakimsikiliza kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi Mhandisi Consolata Ngimbwa akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa,Viongozi wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi  na Wajumbe waliohudhuria mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 nje ya  ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Wakandarasi Wanawake mara baada ya kufungua Mkutano wa siku mbili wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...