Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera.


WAKAZI wa Mkoa wa Kagera wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya soko kuu la Manispaa ya Bukoba kwenye zoezi la upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza bure.

Zoezi hilo linakoratibiwa na ofisi za mfuko wa bima ya afya(NHIF)Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na ofisi za makao makuu ya mfuko huo linatafanyika kwa muda wa wiki nzima.

Meneja wa mfuko wa Bima ya afya Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo alisema kuwa zoezi hilo la upimaji afya litahusisha magonjwa yasiyoambukiza kama shinikizo la damu(BP),Sukari,macho,uzito na urefu pia watakaokutwa na matatizo watapewa ushauri wa kitaalam.

Odhiambo alisema kuwa zoezi hilo ni sehemu ya majukumu ya mfuko wa NHIF ya kuhudumia wananchi lakini wanaendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo wa matibabu ili wawe na uhakika wa matibabu pale wanapougua wao na familia zao.

Alisema lengo lao ni kuwafikia wananchi zaidi ya elf moja katika maeneo ya Manispaa ya bukoba hivyo aliwataka wananchi wa Bukoba kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la kupima afya zao.

Mgeni rasmi katika ufunguzi wa zoezi hilo Mkuu wa Wilaya ya Muleba Injinia Richard Ruyangu aliwataka wananchi wote kujiunga na mfuko wa bima ya afya ili kuwa na uhakika wa matibabu pale wanapougua wao na familia zao.

Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Muleba akipima afya katika uzinduzi wa zoezi la upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza linaloratibuwa na mfuko wa bima ya afya NHIF Kagera.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa zoezi la upimaji afya bure wa magonjwa yasiyoambukiza Mkuu wa Wilaya ya Muleba Injinia Richard Ruyango akiongea na wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo(hawapo pichani).
Meneja wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akiongea jambo wakati wa zoezi la ufunguzi wa upimaji afya bure kwa magonjwa yasiyoambukiza kwa wakazi wa manispaa ya bukoba.


Baadhi ya wakazi wa manispaa ya bukoba waliojitokeza kupima afya zao wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani)katika uzinduzi wa zoezi hilo.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...