Na Fredy Mgunda, Iringa.

Wananchi wa kijiji cha uhambila wilayani Mufindi Mkoani Iringa wametakiwa kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji na maliasili zilizopo katika kijiji hicho.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara wa kijiji hicho Afisa mradi kutoka shirika la LEAT upande wa wilaya ya mufindi Jamali Juma alisema kuwa wananchi wanatakiwa kujiepusha na ukataji miti hovyo na kulima vinyungu kwenye vyanzo vya maji kwa kuwa kufanya hivyo kunasababisha ukame.

“Mkiangalia zamani maeneo haya yalikuwa ya kijani na tulikuwa na mito midogo midogo mingi iliyokuwa inatililisha maji msimu mzima lakini hali ya sasa haipo hivyo kutokana na kutaka miti na kuaharibu vyanzo maji nawaomba wananchi acheni hiyo tabia ili tuwe na Mazingira mazuri kama zamani”alisema juma

Ukataji miti na uharibifu wa vyanzo unasababisha madhara mengi makubwa na ndio maana tunaona sasa kumekuwa na magonjwa mengi ambayo yanaathari ya moja kwa moja kwa mwanadamu lakini pia uharibifu huo husababisha mabadiliko ya vipindi vya mvua na kukosekana kwa mvua za kutosha.

Juma alisema kuwa dunia kwa sasa inakabiliana na swala la mabadiliko ya tabia nchi hata hivyo wananchi mnatakiwa kuwa umakini ili msije mkaishi kwenye jangwa kutokana na uharibifu wetu.

“Ni kosa la jinai kwa mtu yoyote yule kukata miti bila kibali au kuharibu vyanzo vya maji kutokana na sheria zetu za mwaka 1982 hivyo kukata miti au kuaribu vyanzo vya maji sio haki ya msingi ya mwananchi” alisema Juma

viongozi wa shirika la LEAT pamoja na viongozi wa kijiji cha Uhambila wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wakati wa kujadili maswala ya utunzaji wa Maliasili na vyanzo vya maji vilivyopo eneo hill.
Baadhi ya wananchi wakisikiliza kinachoendelea kwenye mkutano wa kijiji wa kujadili maswala ya utunzaji wa vyanzo vya maji pamoja Maliasili za kijiji hicho.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...