THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WANANCHI WILAYANI MBOGWE MKOANI GEITA WAPOKEA KWA KISHINDO ZOEZI LA USAJILI WA VYETI VYA KUZALIWA KWA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO

Kata ya Iponya Wilayani Mbogwe,mkoani Geita,imevuka lengo la uandikishaji watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwa ajili ya kupatiwa vyeti vya kuzaliwa kwa zaidi ya watoto 900 sawa na 154.7%

Kauli hiyo ilitolewa na mratibu wa zoezi la usajili wa watoto chini ya umri wa miaka mitano wa wilaya ya Mbogwe,Fredrick Chotamasege, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya hali ya uandikishaji kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe aliyefanya ziara ya ufuatiliaji katika kata ya Iponya.

“Kata ya Iponya imefanikiwa kuvuka lengo katika zoezi la uandikishaji watoto chini ya umri wa miaka mitano zoezi linaoendeshwa na wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA). Kata ya Iponya iliwekewa lengo la kuandikisha watoto 1,806 lakini hadi kufikia tarehe 16/05/2017 ilikuwa imeandikisha watoto 2,794” alisema Fredrick. Aliongeza kuwa usajili huo ni sawa na ongezeko la watoto 988 waliosajiliwa sawa na 54.7%.

Pamoja na mafanikio makubwa ya zoezi hilo,zipo changamoto za mawasiliano ya mtandao wa Tigo unaotumika kutuma takwimu hizo. Aliongeza kuwa mtandao huo umekuwa ukitumia muda mrefu kutuma majina na hivyo kusababisha kuwa na takwimu tofauti kati ya zile zilizopo kwenye vitabu na zile za kwenye mtandao wa RITA.

Haya yalielezwa wakati Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Elias Kayandabila, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya zoezi la uandikishaji watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika kata za Masumbwe na Iponya wilayani Mbogwe.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA