Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Watu wawili, Ally Sadick na Anna Kimaro, wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kuharibu mali ya milioni 47.

Hata hivyo, washtakiwa watatu wanaodaiwa kutenda kosa pamoja na hao hawakuweza kufika mahakamani na bado wanatafutwa.

Wakili wa Serikali, Patrick Mwita amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa washtakiwa hao ni Omary Sadick, Tumsifu Kimaro na Steven Kimaro ambao wanaendelea kutafutwa ili waweze kukabiliana na kesi hiyo.

Katika kesi hiyo imedaiwa kuwa, huko katika eneo la Kunduchi Mtongani wilaya ya Kinondoni washtakiwa waliharibu nyumba mbili, choo na miti ya minazi mitatu vyote vikiwa na thamani milioni 47 mali ya Mohamed Mshindo.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, walikana na upelelezi bado haujakamilika.

Mahakama imewaamuru washtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao kila mmoja asaini dhamana milioni 10.

Kesi imeahirishwa hadi Juni 13, mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...