THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAWILI WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA YA BIASHARA YA MENO YA TEMBO

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Watu wawili wanashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na nyara za serikali za Meno ya Tembo vipande sita ambavyo vilivyokamatwa Chanika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Somon Sirro amesema kuwa  vipande hivyo vilikamatwa wakati polisi wakifanya operesheni kupata taarifa ya watu wanataka kufanyabiashara ya kuuza vipande sita vya meno ya tembo na kwenda kuwatia hatiani nje ya nyumba ya moja ya watuhumiwa hao.

Watuhumiwa hao ni Mfanyabiashara Senei Abbas (36) pamoja na  Juma Mkong’wa (33) Fundi Ujenzi Mkazi wa Gongolamboto  jijini Dar es Salaam.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi linamshikilia Mwanafunzi wa Chuo cha St. Joseph, Lewis Mbise (23) kwa tuhuma za kukutwa na silaha aina ya Luger CZ yenye namba za usajili C 4122 ikiwa na risasi 13 ndani ya magazine .

Mwanafunzi huyo alipohojiwa alivyopata silaha na kukiri kuwa aliiba kwa baba yake pamoja na fedha Tasilimu sh.800,000.
Jeshi polisi limeagiza kukamatwa kwa baba wa manafunzi kwa kukosa kutunza silaha mpaka mwanae anapata nafasi ya kwenda kuiiba.
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi inawashilikilia watu watatu kwa tuhuma za kuvujisha mtihani wa kidato cha Sita ambao unafanyika hivi sasa.

Watuhumiwa hao ni Mwalimu  Mussa Elius , Mwalimu Innocent Mrutu pamoja na mwanafunzi wa Kidato  cha Sita, Ritha Mosha .
Kamanda Sirro amesema wanaaendelea na mahojiano kuhusiana na mtihani  wa kidato cha sita unaoendelea kufanyika.

Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa watatu ambao ni walinzi kituo cha Mafuta cha Camel Kurasini kwa kula njama za wizi wa mauta lita 36000 zenye thamani ya sh. Milioni 72.

Walinzi hao Hamis Peter (49) mkazi wa Charambe, Jumanne Hamis (35) pamoja na Huruka Ramadhan (37).
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake jijini Dar es Salaam  leo. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akionyesha vipande vya meno ya tembo vilivyokamtwa na jeshi hilo leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akionyesha silaha waliokamata kwa mwanafunzi ambayo aliiba kwa baba yake  leo jijini Dar es Salaam.