THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WAZIRI CHARLES MWIJAGE AFUNGUA MAONYESHO YA TANO YA KIMATAIFA YA BIASHARA TANGAMeneja Mkuu Idara ya Masoko kiwanda cha saruji cha  Rhino Tanga, William Malonza, akimuonyesha moja ya bidhaa zizalishwazo na kiwanda hicho, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage, wakati wa maonyesho ya tano ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika  katika viwanja ya maonyesho Mwahako ambayo yamezishirikisha kampuni kutpka mataifa mbalimbali ya Barani Afrika na Asia.


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage, akisalimiana na Afisa Masoko kiwanda cha saruji cha  Rhino Tanga, Carolina Hillary wakati alipotembelea banda la maonyesho ya tano ya Kimataifa yalifunguliwa leo jijini Tanga katika viwanja vya maonyesho Mwahako.

 Waziri wa viwanda na Biashara, Mhe. Chales Mwijage, akibadilishana mawazo na Meneja Mkuu Idara ya Masoko kiwanda cha Saruji cha Rhino Tanga, Bw. William Malonza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika Tanga.
 Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijaga akipata maelekezo ya namna mkonge unavyoweza kutengeneza dawa  pamoja na mafuta aina mbalimbali.
 Simba ni moja katika wanyama ambao wameletwa kwa ajili ya maonyesho hayo ya Tanga. Wapo katika banda la idara ya Wanyamapori.