Na Husna Said & Nuru Juma- MAELEZO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uelewa juu ya ualbino yatakayofanyika Juni 13 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. 

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania Nemes Colman Temba alipokutana na waandishi wa habari. 

Temba alisema maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kuibua mijadala na tafakuri kwa wadau juu ya ukusanyaji endelevu wa takwimu,uchambuzi na upatikanaji wa watu wenye Ualbino kwa wakati ili Serikali iweze kuwasajili, kuwahudumia na kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wanakuwa salama.

“Bila ya utaratibu mzuri wa upatikanaji wa Takwimu Serikali haitaweza kupanga vyema juu ya ustawi wa watu wenye ualbino, hivyo maadhimisho ya mwaka huu yataibua mjadala wa umuhimu wa upatikanaji wa takwimu sahihi kutoka ofisi ya Taifa ya takwimu kwaajili ya kusaidia katika mipango ya maendeleo ya watu wenye ualbino”,alisema Temba.

Aidha alisema Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 iliyojumuisha takwimu za watu wenye ualbino ilisaidia kubaini idadi ya watu hao ambapo walikuwa 16,376 wakiwemo Wanaume 7,620 na Wanawake 8,756.
Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) Bw. Nemes Temba (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uelewa juu ya ualbino mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaam Bw.Gabriel Aluga na kushoto ni Afisa Mawasiliano na Habari wa chama hicho Bw. Josephat Torner.
Afisa Mawasiliano na Habari wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) Bw. Josephat Torner (katikati) akifafanua jambokwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uelewa juu ya ualbino mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Bw. Nemes Temba na kushoto Mwekahazina wa chama hicho Bw. Abdulah Omar.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) Bw. Nemes Temba (mwenye koto jeusi) wakati akielezea maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu wa ngozi mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Eliphace Marwa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Miss Tanzaia mwaka Huu wawe walemavu tuu wangozi wakiongozwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...