Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 
 WAZIRI Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema Serikali imejipanga katika kuimarisha sekta ya kilimo hili kuimarisha sekta ya Viwanda nchini. 
Amesema hayo alipokuwa akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyabiashara nchini Ikulu jijini Dar es Salaam Jumamosi wakati akijibu hoja mbalimbali juu ya upatikanaji wa mbolea na malighafi. “Tayari kuna kiwanda cha utengenezaji matrekta hapahapa nchini kinajengwa pale Kibaha (mkoa wa Pwani) hivyo gharama za ununuaji wa matrekta utapungua na yatakuwa yanapatikana kwa urahisi hili kuweza kuboresha kilimo kwa sekta hii ambayo ni tegemeo kubwa katika kuimarisha uchumi wa viwanda” amesema Waziri Mkuu.
Ameeleza kuwa katika uimarishaji wa uzalishaji mazao mashambani tayari serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha kumpa mzabuni mmoja awe ndio muagizaji mkuu wa mbolea za DAP na UREA hili kuondoa urasimu wa bei kwa wakulima. 
Ametaja kitendo cha kila wakala kuagiza mwenyewe mbolea kumepelekea bei ya mbolea kutofautiana nchi nzima hali inayochangia katika kuzorota kwa uzalishaji mashamabani kwa mbolea kutofika kwa wakati. 
Mhe. Majaliwa pia amesema ofisi yake inafanya mapitio upya ya tozo za mbolea ili kuweza kupunguza gharama kwa mkulima kwani aoni haja ya kuwepo kwa tozo mbalimbali kwenye mbolea ambazo zinamkandamiza mkulima moja kwa moja. 
Amesema kuwa moja ya jitihada zingine za kumsaidia mkulima nchini ni pamoja na ufunguzi wa benki ya kilimo ambayo wakulima wataweza kunufaika na mikopo mbalimbali ambayo itakuwa ikitolewa na benki hiyo. 
 Aidha Waziri Mkuu Majaliwa alitumia fursa hiyo kuwaambia Wafanyabiashra hao kuwa serikali inatambua mchango wa sekta binafsi na ipo pamoja nao na kusema anawashukuru wafanyabiashara hao wanavyotambua kwa jinsi gani serikali ilivyopambana na rushwa katika maeneo mbalimbali ya kazi.
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara katika  ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam . Kushoto kwake ni Waziri  
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TSPF) Dkt. Reginald Mengi, Rais Dkt John Pombe Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu ) Mhe. Jenista Mhagama

 Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba  Akizungumza katika
mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara katika  ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam

Wajumbe  katika mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara katika  ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...