THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAZIRI MKUU: SERIKALI KUCHIMBA MABWAWA YA MAJI ILI KUPUNGUZA UHABA WA MAJI NCHINI.

Na Husna Saidi.

SERIKALI imesema imeandaa mpango kabambe wa uchimbaji wa mabwawa ya kutiririsha maji ya mvua katika baadhi ya maeneo nchini ili kupunguza hadha ya ukosefu wa maji kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo na Wazirti katika kikao cha Bunge la bajeti linaloendelea Mjini Dodoma.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema katika kutekekeleza mpango wa Serikali kumtua “Mama ndoo kichwani” Serikali imedhamiria kupunguza umbali mrefu wanaotumia wananchi kutafuta maji, ambapo imepanga kuchimba mabwawa makubwa ya maji katika  maeneo ambayo yana mtiririko wa maji.

“Tutaendelea kutoa maelekezo kwa Watendaji wetu kuhamasisha wananchi kutumia fursa ya misimu wa mvua ili kujiwekea akiba ya maji ambayo yatawasaidia wakati wa kipindi cha kiangazi hususani katika maeneo ambayo yana uhaba wa maji”.

Kwa mujibu wa Majaliwa alisema katika Bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Serikali imeandaa mpango maalum wa uchimbaji wa mabwawa ya maji sambamba na kufanya ukarabati wa mabwawa ambayo yameharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa alizitaka Halamashauri zote nchini kuhakikisha zinatumika vyema mabwawa na mifereji iliyokuwa katika maeneo ili kuweza kuvuna maji ya mvua na kuyahifadhi kwa msimu huu wa mvua na ujao.

Majaliwa aliongeza kuwa Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya mabwawa yote nchini ili kuhakikisha halmashauri zote nchini zinakuwa na utoshelevu wa huduma ya maji kwa wananchi wake.

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akijibu maswali Mbalimbali ya Wabunge katika kikao cha Ishirini na mbili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11, 2017.