Na
Lorietha Laurence
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameupongeza uongozi wa Klabu ya michezo ya
Afrika Lyon kwa kutumia mchezo wa mpira
wa miguu kuelimisha jamii kupambana na ujangili wa tembo.
Waziri
Mwakyembe ametoa pongezi hizo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na
uongozi wa klabu hiyo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Idara ya
Habari MAELEZO.
Katika
kikao hicho uongozi wa timu hiyo ulimueleza Waziri kuwa timu yao imeamua
kushiriki vita dhidi ya vitendo vya mauaji ya tembo kwa kuandika ujumbe maalum
katika jezi za timu hiyo kuelimisha jamii dhidi ya vitendo hivyo.
“ni
jambo zuri kuhakikisha jamii inapata burudani ya mpira wakati huo huo inaelimika
kupitia ujumbe unatolewa na wachezaji katika jezi zao”Dkt Mwakyembe alisema.
Kwa
hivyo, aliushukuru uongozi wa timu hiyo kwa juhudi zao hizo na kukieleza
kitendo hicho kuwa ni “cha mfano na kujivunia”.
Aliongeza
kuwa Serikali inajivunia na kuthamini mchango wa wananchi wazalendo
wanaojitolea kujenga taifa na kulinda rasilimali zake kama timu ilivyofanya
timu hiyo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akipokea jezi kwa niaba ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya afrika Lyon Bw.Rajuu Kagenzi (kushoto) mara baada ya kikao na uongozi huo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akionyeshwa michora ya ramani za viwanja vya michezo vinavyotarajiwa kujengwa kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya afrika Lyon Bw.Rajuu Kagenzi (kushoto) leo Jijini dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...