THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAZIRI MWIGULU NA WATENDAJI WAKE WAKUU WAJADILI BAJETI YAKE IKIWA NI MAANDALIZI YA MWISHO KABLA YA KUIWASILISHA KWENYE BUNGE LA BAJETI MJINI DODOMA JUMANNE

 Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Lameck Nchemba  wa pili kushoto akitoa Maelekezo kwa  Watendaji Wakuu wa  Wizara yake wakati wa Kikao cha cha maandalizi ya mwisho cha kupitia Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara yake, kabla ya kuiwasilisha Bajeti ya Wizara yake katika Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Jumanne. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamadi Masauni na wa kwanza kulia ni  Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Wizara mjini Dodoma. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu aliyenyanyua mkono akitoa ufafanuzi wa jambo fulani kuhusu bajeti  ya Jeshi la Polisi nchini mbele ya Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba  wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni maandalizi  ya mwisho kabla ya Bajeti ya Wizara hiyo kuwasilishwa kwenye  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,siku ya  jumanne.Kikao hicho kilichowashirikisha Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo na Maafisa Mipango wa Wizara kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  wizara hiyo mjini Dodoma. 
 Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba  akipokea taarifa mbalimbali zilizotolewa na watendaji wakuu wa Wizara yake wakati wa Kikao cha Maandalizi ya mwisho ya kupitia ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara yake,  kabla ya kusomwa kwa Bajeti ya Wizara yake katika Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Jumanne. Kushoto kwake ni  Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamadi Masauni, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  wizara mjini Dodoma. 
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza  nchini, Dkt. Juma Malewa wa pili kulia akitoa ufafanuzi mbele ya Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba  wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni maandalizi  ya mwisho kabla ya Bajeti ya Wizara hiyo kuwasilishwa kwenye  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,siku ya Jumanne.Kikao hicho kilichowashirikisha Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo na Maafisa Mipango wa Wizara kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Wizara hiyo mjini Dodoma. 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye wa tatu kulia  akitoa ufafanuzi kuhusu Jeshi lake mbele ya Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba  wakati wa Kikao cha maandalizi ya mwisho ya kupitia ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  kabla ya Bajeti ya Wizara hiyo kusomwa kwenye Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,siku ya Jumanne.Kikao hicho kilichowashirikisha Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo na Maafisa Mipango wa Wizara kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Wizara hiyo mjini Dodoma. 
PICHA ZOTE NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI