Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar.

Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo amesema tatizo la kuharibika kwa mashine ya kusagia taka katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja siku za karibuni kulipelekea kurundikana kwa taka na kusababisha usumbufu kwa wananchi.

Amesema baadhi ya wafanyakazi wakorofi wa Hospitali hiyo walitumia kasoro hiyo kuzitupa taka kwenye ufukwe wa bahari, nyuma ya Hospitali, ambapo ni kosa kwa mujibu wa sheria na kanuni za afya na uhifadhi wa mazingira.

Waziri Mahmoud ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kutembelea mashine ya kusagia taka zinazozalishwa katika Hospitali hiyo ambayo hivi sasa imefanyiwa matengenezo na ipo tayari kufanyakazi na kuondosha kero hilo.

Amesema wafanyakazi saba waliobainika kufanya kosa la kutupa taka sehemu ya ufukwe wamechukuliwa hatua za nidhamu na kuuagiza uongozi wa Hospitali ya Mnazimmoja kutomvumilia mfanyakazi atakaekiuka kanuni za afya.

Hata hivyo Waziri wa Afya amekiri kuwa uzalishaji wa taka katika Hospitali ya Mnazimmoja umekuwa mkubwa kutokana na ongezeko kubwa la wagonjwa baada ya kutanuliwa na kufikia daraja la kuwa Hospitali ya rufaa.
Waziri wa Afya Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akipata maelezo ya mashine mpya ya kusagia taka za hospitali kwa Mtaalamu wa mashine hizo kutoka Kenya Benard Abere. Picha na Makame Mshenga. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...