Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi ametembelea Ubalozi wa Tanzania Nairobi Kenya na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Mheshimiwa Balozi Mteule Dkt. Pindi Hazara Chana.

Prof. Kabudi alifanya ziara hiyo tarehe 4/5/2017 wakati akihudhuria Mkutano wa 56 wa Mwaka wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria ya Nchi za Asia na Afrika (Asian-African Legal Consultative Organisation –AALCO) unaofanyika mjini Nairobi.

Katika ziara hiyo Prof. Kabudi aliongozana na Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda Balozi Mteule wa Tanzania Nchini India yalipo makao makuu ya Jumuiya hiyo na maafisa wengine wa Wizara ya Mambo ya Nje.

Prof. Kabudi alimpongeza Balozi Pindi Chana kwa uteuzi na alishukuru kwa maandalizi waliyoyafanya kuhakikisha ujumbe wa Tanzania unashiriki ipasavyo mkutano huo. Vile vile alimuhakikishia kuwa Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na taasisi zake zitampa ushirikiano stahiki katika utekelezaji wa majukumu yake, na kwamba Ubalozi uwe tayari kwa kufuata taratibu zilizopo kiserikali kuwasiliana na Wizara pindi yanapoibuka masuala yanayohitaji ushiriki wa Wizara.

Kwa upande wake Balozi Dkt. Pindi Chana alimshukuru Prof. Kabudi kwa kutenga muda kuja kuutembelea Ubalozi na kumpongeza kwa uteuzi alioupata. Balozi Chana alimuahidi Prof. Kabudi kuwa Ubalozi utaendelea kushirikiana ipasavyo na Wizara kwa kutumia taratibu zilizopo utahakikisha kuwa masuala ya Wizara yanaifikia Wizara kwa wakati. 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...