Kampuni ya simu inayoongoza kwa huduma za vifurushi vya intaneti, Zantel imeanzisha huduma mpya ya vifurushi vya bure kwa wateja wake ikiwalenga zaidi vijana, ambapo tafiti zinaonyesha ndio watumiaji wakubwa wa mitandao ya kijamii.

Akizindua rasmi huduma hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Bw. Benoit Janin amesema wateja wa Zantel wanaojiunga na vifurushi vyetu vya kila siku, wiki na mwezi watapata nafasi ya kutumia mitandao ya Facebook, Twitter pamoja na huduma ya kusikiliza muziki bure kwenye application ya ‘Mdundo.com’.

Aliongeza kwa kusema “Tunajisikia fahari kubwa sana kuweza kuzindua huduma hii mpya ikiwa ni mwendelezo wa jitihada zetu za kupanua na kutoa huduma za kibunifu na kuhakikisha wateja wetu wanaendelea kufurahia mtandao wetu wa Zantel wenye huduma ya intaneti ya kasi zaidi ya 4G Tanzania nzima.

Akifafanua zaidi kuhusu huduma hiyo, Mkuu wa kitengo cha huduma ya Vifaa na intaneti Zantel, Hamza Zuberi alisema, “Kwa wateja wa Zantel watakaonunua vifurushi vya siku, wiki na mwezi ambavyo ni ;-Sh.500/= kwa 500MB, Sh.1000/= kwa 1.2GB, na Tsh.1500/= kwa 2.5G watapata nafasi ya kufurahia huduma hizo za bure. Huduma hizi ni kwa wateja wenye simu au vifaa vyenye uwezo wa kupokea huduma ya intaneti. Kwa wateja wetu wanaotumia simu au vifaa visivyo na uwezo huo wanaweza kujipatia simu au vifaa hivyo kwa gharama nafuu kabisa katika maduka ya Zantel jijini Dar es Salaam na visiwani Zanzibar ili na wao waweze kufurahia ofa hii”.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii uliofanywa na kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwanufaisha hasa vijana ambapo pia wateja wa Zantel watapata huduma ya kusikiliza muziki kwenye Application ya Mdundo.com bure. Kulia ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa Zantel Rukia Mtingwa. 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akigawa Modem kwa wanafunzi wa Chuo cha usimamizi wa fedha cha IFM katika hafla ya uzinduzi wa vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii uliofanywa na kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwanufaisha hasa vijana, ambapo pia wateja wa Zantel watapata huduma ya kusikiliza muziki kwenye Application ya Mdundo.com bure. Anayeshuhudia katikati ni Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti Zantel, Hamza Zuheri. 
Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti Zantel, Hamza Zuheri (kulia) na Meneja wa Muziki na uendeshaji Mdundo.com, Prisna Nicholaus wakimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin (wa pili kulia) Application ya Mdundo.com ambayo wateja wa Zantel wataipata bure baada ya kujiunga na huduma mpya ya vifurushi vya bure kwenye mitandao yote ya kijamii iliyozinduliwa na Kampuni ya Zantel jana jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa Zantel Rukia Mtingwa. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...