Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar.

Hospitali na Vituo vya Afya vya Wilaya vinaweza kupunguza idadi ya akinamama kujifungulia Hospitali kuu ya Mnazimmoja iwapo juhudi za kuandaa mazingira mazuri zitachukuliwa na wakunga na wauguzi  wa vituo hivyo.

Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo ameeleza hayo katika maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Wasanii Rahaleo.
Amesema akinamama  wengi wamejenga imani ya kujifungua  Hospitali kuu ya Mnazimmoja na kupelekea upungufu wa nafasi katika Hospitali hiyo huku vituo vya Afya vijijini vikiwa na akina mama  wacheche wanaokwenda kwa huduma ya kuzaa.

Ameongeza kuwa Hospitali ya Mnazimmoja inazalisha zaidi ya akinamama 50 kwa siku na Mwembeladu wanawake 30 wengi wao kutoka vijijini wakati vituo vya afya vya huko vinazallisha wanawake wawili hadi watano kwa siku.
Waziri Mahmoud amewataka wakunga na wauguzi wa vituo vya afya vya Wilaya vinavyotoa huduma ya kuzalisha  kuandaa mazingira yatakayowavutia wanawake kujifungua katika vituo vyao.

Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea na mkakati wa kuandaa mazingira mazuri na kuweka miundo mbinu bora  ikiwemo vifaa vya kisasa hivyo amewataka wafanyakazi nao kubadilika na kuwapa faraja wagonjwa ili wajenge imani kwao.
 Brass band ya Chipikizi ikiongoza maandamano ya wakunga na wauguzi kupita mbele ya mgeni rasmi Waziri Afya Mhmoud Thabit Kombo katika maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Wasanii Rahaleo Mjini Zanzibar. 
  Mama Mariyam Othmani Mihale akiongoza wakunga na wauguzi katika wimbo maalum wa maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani katika ukumbi wa Wasanii Rahaleo.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wuguzi na Wakunga Zanzibar Amina Abdulkadir Ali akitoa maelezo juu ya siku ya Wuguzi duniani katika maadhimisho yaliyofanyika ukumbi wa wasanii Rahaleo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...