Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN), Dkt.  Jim Yonazi akijibu hoja mbalimbali ambazo ziliibuliwa katika kongamano la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika leo mjini Dodoma . TSNwalikuwa mmoja wa wadhamini. Dk Yonazi alisema kuwa ili kuwaezesha wananchi kiuchumi ni lazima jamii ihabarishwe juu ya fursa mbalimbali zilizopo, lakini pia muhimu wa sekta binafsi kuwa na ubunifu na mifumo ya kujitengenezea utajiri.

Afisa Mtendaji Mkuu wa MM Maxcom , Juma Rajab akielezea uzoefu wake na kusema kuwa inahitajika kuwawezesha wajasiriamali wote, wadogo, wa kati na wakubwa ili kufanikisha wananchi kuweza kuingia katika uchumi wa viwanda.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akitoa mada juu ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi ambapo alisema ni vyema viongozi na jamii ikawana na utaratibu wa kuchapa kazi ili iweze kufanikiwa katika suala la uwezeshaji wananchi kiuchumi.
.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala akisalimiana Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira walipokutana katika Kongamano la pili la  Uwezeshaji wananchi Kiuchumi mjini Dodoma.
 Dk. John Kyaruzi kutoka SAGGOT CTF akitoa mada na kuweka wazi kuwa taasisi hiyo iko vizuri kuwawezesha wananchi. Aidha alisema ni vyema sasa wananchi wakalazimishwa kulima kibiashara tofauti na ilivyo sasa. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...