NA MWANDISHI WA K-VIS BLOG
WATU wasiojulikana wamechoma msitu wa Kirando wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa ambao umeunguza miundombinu ya umeme ya Shirika la umeme Nchini TANESCO.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jioni hii Juni 24, 2017 na Kaimu Meneja Uhusinao wa TANESCO makao Makuu, Bi. Leila Muhaji, imesema, uharibifu huo mkubwa wa miundombinu umeathiri upatikanaji wa umeme kwa wateja wa maeneo ya Kirando na Kipili wanaopata huduma ya umeme ya njia ya msongo mkubwa wa umeme unaopita kwenye maeneo hayo.
“Mafundi wa TANESCO waliofika kwenye eneo hilo, wameshuhudia uharibifu mkubwa ambapo miundombinu ya umeme imeungua na kusababisha hasara kubwa.” Alisema Bi Leila katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Bi Leila amesema TANESCO inawaomba wananchi wote waishio kwenye maeneo hayo kutoa taarifa kwenye ofisi za TANESCO au kituo cha polisi kilicho karibu ili kuokoa miundombinu ya umeme kwa manufaa ya taifa.
Amesema, tayari vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na TANESCO wameanza msako ili kuwabaini wahusika ili sheria ichukue mondo wake.

Uharibifu mkubwa ambapo miundombinu ya umeme imeungua na kusababisha hasara kubwa na kuathiri upatikanaji wa umeme kwa wateja wa maeneo ya Kirando na Kipili wilayani Nkasi, mkoa wa Rukwa
 Afisa wa polisi akiwa eneo la tukio huku akishuhudia jinsi moto huo ulivyoathiri nguzo za umeme
Uharibifu mkubwa ambapo miundombinu ya umeme imeungua na kusababisha hasara kubwa wilayani Nkasi, mkoa wa Rukwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...