Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikian na DTBi wametoa mafunzo kwa walimu wa shule za msingi na sekondari ikiwa ni katika matayarisho yakufungua maabara ya kompyuta yanayotegemea kuzinduliwa mwezi huu.

Mafunzo hayo yametolewa na walimu 6 toka katika Kituo cha Elimu cha Galway nchini Ireland kwa lengo la kuwapatia uwezo , mbinu na maarifa ya technoologia ya kompyuta ili kuweza kuwafundisha wanafunzi watakaojiunga na kutembelea maabara hiyo ujuzi utakaowawezeshaa kutengeneza program ndogo ndogo na baadaye kuweza kuvumbua program kubwa zenye kuleta suluhisho kwa mahitaji mbalimbali ya biashara na jamii.

Maabara ya Airtel Fursa itatatoa fursa kwa vijana wenye malengo ya kujifunza masomo ya Tehama kuongeza ujuzi, na kutoa mwanga kwa vijana kuwa wabunifu kwa kuzindua application mbalimbali ambazo zitaweza kuwaingizia kipato.

Akiongea wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), George Mulamula alisema “ kutokana na changamoto iliyopo kwa sasa ya wanafunzi wengi kutumia kompyuta kwa mara ya kwanza wanapoingia katika elimu ya chuo kikuu kumefanya kuwe na ufinyu katika ubunifu na kutumia technologia katika ujasiriamali. Tunaamini maabara ya Airtel Fursa yatatoa mwaya kwa vijana kujifunza masomo na kuvumbua mambo mengi wakiwa katika umri mdogo.

Mafunzo haya kwa walimu tunayotoa leo ni uthibitisho wa dhamira yetu katika kuhakikisha tunakuwa na walimu bora watakaowasaidia wanafunzi kujikita kwenye technologia na kuwa wabunifu. Aliongeza Mulamula.

Kwa upande wake Meneja huduma kwa jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi alisema “ tumejipanga kuwawezesha vijana kuzifikia ndoto zao kwa kuanzisha maabara hii yenye kompyuta za kujifunzia na kuwawezesha wanafunzi kujifunza mafunzo mbalimbali yatakayowawezesha kutanua wigo wao”.

kupitia program ya Airtel Fursa tunayo application ya VSOMO iliyotengenezwa na kjana wakitanzania ambao leo hii inawawezesha maelfu ya watanzania kuipakuwa na kusoma masomo ya ufundi ya VETA kupitia simu zao za mkononi. Tunaamini maabara hii itakuvumbua na kukuza zipaji vingi na kuleta uvumbuzi katika Tehama. Aliongeza Bayumi.
Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), George Mulamula (wa tatu kulia), akikabidhi cheti kwa Mwalimu wa Kompyuta wa Sekondari ya Loyola, Sista Maria Sany, baada ya kuhitimu Mafunzo ya Walimu katika fani ya sayansi kwa kutumia programu za kompyuta ili kuwawezesha kufundisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, yaliyofadhiliwa na Airtel Tanzania na kuwezeshwa na Kituo cha Elimu cha Galway cha Ireland, katika Shule ya Msingi Kijitonyama jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa nne kulia), Mkurugenzi wa Galway, Bernard Kirk (wa pili kulia) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Beatus Amri.
Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), George Mulamula (wa tatu kulia), akikabidhi cheti kwa Mwalimu wa Sayansi wa Shule ya Msingi Kijitonyama, Magdalena Mtei, baada ya kuhitimu Mafunzo ya Walimu katika fani ya sayansi kwa kutumia programu za kompyuta ili kuwawezesha kufundisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, yaliyofadhiliwa na Airtel Tanzania na kuwezeshwa na Kituo cha Elimu cha Galway cha Ireland, yaliyofanyika shuleni hapo, jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa nne kulia), Mkurugenzi wa Galway, Bernard Kirk (wa pili kulia) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Beatus Amri.
Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), George Mulamula (wa tatu kulia), akikabidhi cheti kwa Mwalimu wa Hisabati na Sayansi wa Shule ya Msingi Kijitonyama, Wilfred Ringo, baada ya kuhitimu Mafunzo ya Walimu katika fani ya sayansi kwa kutumia programu za kompyuta ili kuwawezesha kufundisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, yaliyofadhiliwa na Airtel Tanzania na kuwezeshwa na Kituo cha Elimu cha Galway cha Ireland, yaliyofanyika shuleni hapo, jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa nne kulia), Mkurugenzi wa Galway, Bernard Kirk (wa pili kulia) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Beatus Amri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...