THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

ARUMERU YANUFAIKA NA MITAMBO YA KISASA YA UPATIKANAJI WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA NA TAHADHARIFundi Sanifu Mkuu Bonde la Pangani Bw. Vendelin Basso akionesha namna ya kusoma vifaa vya kupima kina cha maji kwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu (bajeti) Bi. Grace Mosha
Muonekano wa Vifaa vya kisasa vya kupima kina cha maji vilivyofungwa na mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari katika mto Kikuletwa Kijiji cha Kikwe Meru ambavyo husaidia katika taarifa za utabiri wa hali ya hewa na kuchukua tahadhari ya mafuriko. 

Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari Bw.Daniel Alfei akizungumza na baadhi ya wanufaika wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari (hawapo pichani) walipotembelea kufanya tathimini ya utekelezaji wa mradi huo Wilayani Arumeru Juni 09, 2017. 
Baadhi ya wakazi wa Vijiji vya Mbuguni Wilayani Arumeru wakimsikiliza Mratibu Taifa wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari Bw.Daniel Alfei (hayupo pichani) wakati wa tathimini ya utekelezaji wa mradi huo iliyofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu 09Juni, 2017.