Golikipa wa Azam aliyesajiliwa kutoka timu ya Mbao Fc Benedict Haule akiwa ameanza mazoezi na klabu yake ya zamani.

Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC imeanza  rasmi mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao (2017-2018) huku ikiwa imepata mwaliko maalum nchini Rwanda kutoka kwa mabingwa wa nchi hiyo, Rayon Sports.
Awali Azam FC ilipanga kuanza maandalizi ya msimu mpya Jumatatu ijayo Julai 3, lakini kutokana na mwaliko huo imeamua kuanza mazoezi mapema, ambapo Rayon imealika kwa ajili ya kucheza nao mchezo wa kirafiki Julai 8 ikiwa ni sehemu ya kusherehesha ubingwa walioutwaa.
Wachezaji waliofanikiwa kuhudhuria kwenye mazoezi hayo ya kwanza ni pamoja na makipa Mwadini Ally, Benedict Haule, aliyerejea Azam FC kwenye usajili huu akitokea Mbao FC, Metacha Mnata na mabeki Bruce Kangwa, Abbas Kapombe, Ramadhan Mohamed, Abdul Omary.

Viungo ni Frank Domayo, Masoud Abdallah, Stanslaus Ladislaus na mshambuliaji Yahaya Zaidi, huku wachezaji wengine wakiwa na udhuru na baadhi wakiwemo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachoshiriki michuano ya COSAFA, Nahodha Msaidizi Himid Mao ‘Ninja’, kiungo Salmin Hoza na mshambuliaji Mbaraka Yussuf.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, alisema kuwa mbali na mwaliko huo kupelekea kuanza mapema mazoezi, pia sababu nyingine ni kuwaweka fiti zaidi wachezaji ambao hawakuchaguliwa timu ya Taifa ili watakapoungana na wale walioitwa waweze kwenda sawa.
“Tukapokwenda Rwanda kati ya tarehe 5 hadi 6, tunaweza kupata siku kadhaa za kufanya maandalizi yetu pamoja na kucheza mechi kadhaa kabla ya kurejea nyumbani tayari kabisa kufanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya ligi ya msimu ujao,” alisema.
Cheche alisema amefurahishwa sana na namna alivyowaona wachezaji kwenye mazoezi hayo ya kwanza huku akieleza kufurahishwa na usajili unaoendelea kufanywa na timu hiyo mpaka sasa na sera ya klabu ya kupandisha wachezaji kutoka Azam Academy.
“Maingizo ni mazuri na kilichobakia hivi sasa ni kufanya mazoezi kwa pamoja na kuelewana na wenzao, wajuane kitabia nje na ndani ya uwanja ili waweze kushirikiana ma kubwa kuweza kulisukuma mbele gurudumu hili la Azam FC,” alisema.
Azam FC inayodhaminiwa na Benki bora ya NMB na kinywaji safi cha Azam Cola, itaendelea tena na mazoezi kesho saa 10 jioni.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...