MACHO na masikio ya watanzania leo yanahamishiwa kwa muda mjini Dodoma wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango atakapowasilisha bajeti ya pili ya Serikali ya Awamu ya Tano bungeni mjini hapa.

Awali Wizara ya Fedha na Mipango iliwasilisha Bajeti ya kwanza ya Sh 29.5 trilioni iliyoonekana kubana sehemu tofauti tofauti na kusababisha wananchi kulalamika, wengi wakisema mzunguko wa fedha umedhoofika huku biashara zikifungwa.

Bajeti hiyo ndiyo iliyowafanya wachambuzi wa masuala ya uchumi, makundi ya biashara na wabunge kumtaka waziri huyo atangaze hatua mahususi za kuiokoa sekta binafsi na zitakazoharakisha ukuaji uchumi.

Wadau wanatarajia kuwa Dk Mpango, ambaye aliwahi kuwa mchumi mwandamizi katika Benki ya Dunia na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ataangalia kwa kina hali ya sasa ya uchumi na kutangaza hatua za kikodi zitakazozuia kupanda kwa gharama za maisha na wakati huo huo kuipa mkono sekta binafsi ili Serikali ifikie lengo lake kuifanya Tanzania  kuwa nchi ya viwanda.

 Mfumuko wa bei, ambao unahusishwa na kupanda kwa bei za vyakula, tayari umefika asilimia 6.4 kwa mwezi Aprili kutoka asilimia 5.1 mwezi kama huo mwaka jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...