Picha na Habari za Freddy Macha 
 Baadhi yetu huwaita wenye hali hii “taahira” – neno la asili ya Kiarabu  lenye maana “mtu asiye sawa” (wazimu, chizi, bwege, nk).  Sahihi ni “mtindio ubongo” – kwa Kiingereza “Down Syndrome”....
Baadhi ya taswira zake ni : kufikiri na kuzungumza taratibu, kigugumizi,  mwili mfupi,  utofauti wa tambo la kichwa,vidole vya mikono na miguu,nk.
Mbali na kuwanyanyapaa,  jamii zetu Afrika bado hazitambui umuhimu wa kuendeleza wenye ulemavu.
Mwaka huu kijana wa miaka 18, Samwel Mwanyika, mwenye “Mtindio Ubongo “  (Down Syndrome) alikuwa mshindi wa kimataifa wa upigaji picha.
Balozi wetu Uingereza Mheshimiwa Asha-RoseMigiro akaeleza:
“Wametoka vijana wengi kwenye nchi  zilizoendelea, wengine wamemzidi umri...tena wenzetu huwa na mipango maalum ya kuwapa mbinu mbalimbali,...sasa huyu wa familia ya kawaida tu ya Kitanzania ambapo bado hatujaweka miundo mbinu kama walivyoweka huku,  picha yake imeshinda...”
Mwasisi wa kujitolea  wa shirika la Mtindio Ubongo (Pearl of People with Down Syndrome) , Mony Teri Pettite  na wazazi wake Samwel, Philip Mwanyika na Sophie Mshangama, walikutana na Balozi  Migiro na kupongezwa Ijumaa iliyopita. Afisa Utawala Ubalozini, Rose Kitandula , pia alikuwepo.
 Picha ya  Samwel Mwanyika iliyonyakua  tuzo la kimataifa la Stephen Thomas, mjini London.
 Samwel Mwanyika na picha iliyonyakua  tuzo la kimataifa la Stephen Thomas, mjini London.
Balozi Migiro akimvika Samwel Mwanyika bendera ya taifa, alipowakaribisha na familia ofisini kwake, Ijumaa 16, Juni 2017.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...