Na Rhoda Ezekiel Kigoma, 

BARAZA la madiwani halmashauri ya Wilayani Buhigwe limemuondoa rasmi Madarakani aliekuwa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Elisha Bagwanya kufuatia kuthibitishwa kwa tuhuma mbili kati ya saba zilizokuwa zimewasilishwa kwa tume hiyo zikimkabili Mwenyekiti huyo, moja ikiwa ni kutumia vibaya madaraka na kuisababishia hasara halmashauri .

Uamuzi huo umetolewa leo katika viwanja vya Shule ya msingi Buhigwe mara baada ya madiwani wa baraza hilo kupiga kura ya ndio kuunga mkono taarifa ya kamati ya Mkuu wa Mkoa kigoma Brigedia Jeneral Emanuel Maganga, iliyokuwa imebaini ukweli wa tuhuma mbili kati ya saba zilizo wasilishwa na madiwani hao na kumtaka mkurugenzi na Baraza kumuondoa Mwenyekiti huyo.

Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Anosta Nyamoga, alithibutisha kumuondoa mwenywkiti huyo kwa kutangaza matokeo ya kura 20 za ndio na saba za hapana zilizo pigwa na Madiwani wa Halmashauri hiyo .

Nyamoga alisema mnamo tarehe 25 machi alipokea barua kutoka kwa madiwani 20 wa halmashauri hiyo ya kutokuwa na imani na mwenyekiti wa halmashauri na kwa mujibu wa kanuni Na 4(3) ya kanuni za kudumu za Halmashauri,  wajumbe wa Mkutano wasiopungua theluthi mbili wanaweza kuomba kuitishwa kwa mkutano kwa lengo la kujadili agenda ya kumuondoa madarakani mwenyekiti wa halmashauri kutokana na sababu zinazotajwa.

Alisema tume ya mkuu wa mkoa baada ya kupitia tuhuma zote saba zilizotajwa katika barua hiyo ilibaini tuhuma mbili ni za ukweli na zinamnyima Mwenyekiti huyo sifa za kuwa kiongozi, tuhuma hizo ni pamoja na kufanya kazi ya ukandarasi na halmashauri kwa kutumia kampuni yake inayoitwa BUYENZI GENERAL SUPPLIES kwa kazi ya mradi wa maji Nyamugali ambao ni mbovu ,mradi wa Barabara ya Kijiji cha Kigogwe Mrungu,kujenga mradi huo kwa kutumia kampuni ya NGELUKE CONSTRUCTIONS kwa kutumia uwezo wake kama mwenyekiti wa halmashauri na kuzuia miradi hiyo isikaguliwe.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Elisha Bagwanya alievaa suti ya rangi ya Blue 
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya  ya Buhigwe Anosta Nyamoga akiwasilisha taarifa ya tume ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma dhidi ya Mwenyekiti wa halmashauri hiyo

Baadhi ya Madiwani.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...